Mkuu asikudanganye mtu hakuna bank inayoweza kukupa asilimia kubwa unless una mipesa mingi mno. nakushauri uwaona taasisi moja inaitwa UNIT TRUST OF TANZANIA inayoendesha mifuko ya UMOJA FUND, WATOTO FUND, JIKIMU FUND na WEKEZA MAISHA FUND. Wako SUKARI HOUSE GHOROFA YA PILI pale karibu na KILIMANJORO HOTEL(HYATT REGENCY HOTEL). Ukiwekeza katika mifuko hii hutarudi tena kuweka hela yako bank, mfano huo mfuko wa UMOJA FUND unatoa si chini ya asilimia 12 kwa mwaka. siwezi kujibu maswali yote lakini nasisitiza nenda pale sukari house 2nd Floor, au tembelea ofisi zao za mikoani ambazo ziko ndani ya ofisi za posta kuu katika mikoa ifuatayo, DODOMA, MBEYA ARUSHA, MWANZA na ZANZIBAR. Hii ni taasisi ambayo iko chini ya wizara ya fedha. nasisitiza hapo ndo mahali pazuri mana hata mimi nina braza yangu yuko ulaya ila nilimshauri awe anatuma hela anawekeza huko, hajajuta mpaka napoandika post hii, sana sana anaona kachelewa.