Benki za Biashara Tanzania zinaogelea kwenye faida. Je, nini kimefanyika awamu ya sita?

Hakuna miujuzi kwenye kutengeneza faida.

Kwa miaka ya karibuni benk zimejitahidi sana kuboresha huduma na miundombinu yao.

Ile dhana ya financial inclusion imetekelezeka almost 90% kwa sasa. Huku ndipo benk zimejichotea sana fedha.

Kuwepo kwa mawakala,huduma za benk mkononi kuimarika kumefanya watumiaji wapate urahisi.

Kuongezeka kwa gharama za miamala na wingi wa wateja.

Namna nzuri ya utoaji mikopo na ufuatiliaji katika kulipa.

Lakini pia uminyaji wa gharama za endeshaji hizi benki umekuwa mkubwa.

Hii ni pamoja na mishahara duni ya wafanyakazi. Huku uzalishaji ukiwa mkubwa.

Kwa kifupi serikali inamchango mkubwa sana katika kuzifanya hizi benk zifanye vizuri. Janja janja imepungua sana.

Pongezi pia kwa ma CEOs wanapambana kuacha alama.
 
Hebu nyie wajuvi wa JF naomba kuuliza, watumishi wenye mikopo kwenye taasisi za kifedha kwa mwezi januari wameshuhudia mabadiliko kwenye makato yao..yaani mfano unakatwa elfu kumi ili kupunguza deni benki lakini ki mahesabu inaonekana umekatwa elfu 20 bila kuathiri take home ya mtu, je hiyo ni makusudi ya serikali au ni makosa ya ki mfumo?
 
Makato yapo kama awali, hayajabadilika! unless kama ulikuwa na arears!
 
Kweli pesa ipo kwa sasa, Tuchape kazi kwa bidii,
 
Mama anaupiga mwingi kwelikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…