Benki za nmb na crdb miongoni mwa benki 100 bora africa kwa mujibu wa jarida la african business

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
863
Reaction score
408
Jarida la African Business linalochapishwa jijini London Uingereza limetoa orodha ya benki 100 ambazo zimefanya vizuri kwa kipindi cha mwa ka 2012,na miongoni mwao ni benki za NMB na CRDB ambazo zimetajwa katika orodha ya 87 na 94.
Benki tano za Afika kusini ndio zimeongoza orodha hiyo,huku namba moja ikiwa ni Standard Bank Group.
NMB inatajwa kuwa na mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 270(Data za Desemba 2011) na CRDB ikiwa na mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 240(Data za Desemba 2012).
Kwa Afrika Mashariki ni nchi mbili tu ambazo sekta ya kibenki imeonekana kuwa na uimara, ambazo ni Tanzania na Kenya.

Medium Banks Challenge South African Dominance

What bank ranking means for TZ economy - Business - thecitizen.co.tz
 
Tunawapongeza. Ongezeni bidii kwenye hili soko la ushindani bila kusahau kuboresha huduma za wateja (Customer care). Mkumbuke mnashindana na mabenki ya nje yaliyowekeza hapa nchini.
 
Maadam mmeshasema "African business" sina swali..
 
NMB ni sawa kuwa na kiasi hicho kwani inawaibia sana wateja wake ambao wengi wao ni walimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…