Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Wakati taasiai nyingi za kifedha zinananunua madeni ya wafanyakazi ili kuwawezesha kukopa katika taasisi zao, benk za NMB,CRDB na Benki ya Posta hazina kabisa utaratibu huo na hivyo kuwafanya watumishi wanaohiji mikopo kushindwa kupata mikopo mpaka ama waljiipie madeni yao au wasubiri mikopo yao iishe ndio waweze kukopa katika hizo Benki(urasimu).
Faida ya kuchukua mikopo katika benki hizo ni kutokana na ukweli kuwa viwango vyao vya riba ni vya nafuu zaidi ukilinganisha na taasisi zingine za kifedha zinazotoa mikopo ambazo sio za kibenki lakini kikwazo ni huo urasimi wao.
Unaweza kuta mtu amebakiza mkopo kidogo tu na anataka kukopa katika hizo benki ila utashindwa kukopeshwa kwasababu ni lazima deni la taasisi nyingine liishe/lilipwe ili aweze kukidhi sheria ya moja ya tatu jambo ambalo lingewezekana iwapo hizi benki zingekubali kumlipa mtumishi deni hilo na hapo hapo wakamkopesha kwa kumpa kiasi kinachobaki baada ya kuwa wamemlipa deni lake la taasisi zingine za kifedha
Kwa mfano,kama unataka kukopa shilingi 10,000 kutoka benki mojawapo kati ya hizo na ili ukopesheke ni lazima kwanza ulipe deni la shilingi milioni 2 la taasisi nyingine iliyokukopesha awali ndio uweze ukopo ila ikitoke umekwama kupata hiyo milioni 2 basi unashindwa kupata mkopo kutoka NMB,CRDB au Benki ya Posta.
Lakini ukienda katika taasisi zingine zinazotoa mikopo wao wanakuchangamkia na deni wanakulipia na kinachobaki kutoka katika mkopo wako wa milioni 10 waliokukopesha yaani shilingi milioni 8 ndio wanakuingizi kwenye akaunti yako kama take home.
Yaani kwa mfano untaka kukopa milioni 10 ila kiasi unatachopewa ni shilingi milioni 8 tu na milioni 2 waliokukata wanaitumia kukulipia deni la benki au taasisi nyingine ya kifedha ili uweze kukopesheka(waweze kukukopesha hiyo milioni 10) na hivyo unakuwa na mkopo wa taasisi moja tu ya kifedha.
Jambo hili NMB,CRDB na Benki ya Posta kwa sasa haliwezekani kwa maelezo wao hawanunui (hawakulipii madeni ya taasisi nyingine) ili wakukopesha unless usubiri deni lako liishe au ulilipe mwenyewe kama unaweza.
Na zamani ilikuwa ni lazima mshahara upite katika benki yao ndio u-qualify kupewa mkopo ila siku hizi kidogo hilo shariti wamelegeza.
Inawezakana urasimu huu ni kwasababu bado vyuma havijakaza kisawasawa ili hali ikiwa tete urasimu huu wa kutoa mikopo kwa wafanyakazi watauacha.
Sijui na hili mpaka mkuu awaombe walitazame upya kama alivyowaomba kushusha riba za mikopo?!