Benki zitathmini gawio wanalotoa kwa mawakala, wanafanya kazi kubwa

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nimekuwa nikifuatilia hizi huduma

Ni ukweli kuwa, kuna watu wengi wamehamia kufanya huduma zao kwa wakala hasa walioko kwenye bank yetu pendwa na kuacha kabisa kwenda Bank na hata kama wakala yupo mlangoni mwa bank.

Nafikiri Bank inatakiwa KUJITADHMINI HUDUMA ZAKE na sio kuacha kutoa gawio kwa mawakala au kutoa gawio kiduchu huku ikisitisha kutoa machine kwa maana wateja wooote wataishia mitaani.

Hivi inakuwaje mtu asiye na elimu ya bank/fedha aatoe huduma nzuri sana kuliko mfanyakazi wa bank aliyesomea chuoni?
 

Wafanyakazi wa bank wanahisigi zile hela ni zao sijui[emoji28][emoji28]
 
Lililopo ni mawakala kutoa huduma nzuri au ni ukaribu wa kupata hiyo huduma.
 
Ukiachana na huduma ya ATM kwa wakala unatoa zaidi ya laki kwa mara moja tofauti na ATM na laki 4 mara 3 kwa siku.

Hivyo wakala ni bora kuliko BANK
 
Mhudumu bank: Unakaa mtaa gani?
Mimi:Mtaa A
Mhudumu bank: Sasa kudeposit sh elfu 50 unakuja mpaka huku bank uwe anaenda kwa wakala
Mimi🙁 Kwa upole) sawa, ila shughuli zangu nafanyia huku
Mhudumu bank: (tabasamu la kadharau).

Karibu mara mbili wahudumu wa bank wameniambia niwe naenda kwa wakala halafu cha kushangaza tawi lao halina hata wateja na sijawahi kukuta foleni.
Sijui wanataka wawe wanalala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…