Beno Kakolanya ampa makavu mchambuzi uchwara David Felician

Hajafanya jambo LA maana kujibu mambo ya mitandaoni, hiyo ni kazi ya meneja wake.
 
Mechi gani walicheza asubuhi?huyo mchezaji hajitambui, hata mwandiko na reaction yake vinaonesha uwezo wake kichwani
 
Kama aliyeko bench simba anavuta mpunga wa maana kuliko aliyeko golini Yanga shida iko wapi pesa kwanz mengine badae
Atavuta mkwanja ndio, ila atasugua benchi kwa miaka miwili kipaji kitakufa.
Mwisho wa siku mkataba ukiisha anakosa timu anaanza kuzurura mtaani
 
Mechi gani walicheza asubuhi?huyo mchezaji hajitambui, hata mwandiko na reaction yake vinaonesha uwezo wake kichwani
Walicheza Simba seniors na Simba B! Beno alidaka ndio mana jion akacheza Manula, hakuna mchezaji aliyecheza asubuh akacheza na ile ya jion ya mlandege.
 
Atavuta mkwanja ndio, ila atasugua benchi kwa miaka miwili kipaji kitakufa.
Mwisho wa siku mkataba ukiisha anakosa timu anaanza kuzurura mtaani
Kwahiyo akiwa anapata nafasi ya kucheza atacheza maisha yake yote? Wewe unajua Beno ana mipango gani maishani mwake?

Swali jingine:Wewe ukikaa benchi kwa miaka 3 ila mkwanja unaoupata unamzidi mbali mchezaji anayecheza daily kwenye timu X kwa miaka yote mitatu, utaomba uende kwenye hiyo timu X? hayo mambo waliyafanyaga wachezaji wa kizamani ambao walikuwa hawajui hesabu.
 
kutaka kumshambulia personally kunamaanisha anachosema ni sahihi na umekosa hoja za kumjibu.
Dogo ni mpuuzi kitambo na hicho nilichokiandika ni sehemu ya udhaifu wake.

Ana udhaifu wa akili mpaka vitoto vyenzake anavyotembea naye.
 

Mpira vs maisha binafsi.

1. Katika mpira kila mchezaji ndoto yake ni kucheza na kuonekana mara kwa mara, aidha kwenye tv stesheni au moja kwa moja uwanjani. Hakuna mchezaji anayependa akae benchi hata kama unalipwa pesa kiasi gani kwasababu kitendo cha kucheza mara kwa mara kinampa furaha na amani mchezaji, kinakuongezea uwezo wako kimpira, inakujenga kujiamini, kinakuongezea mashabiki, kujulikana, na pia kupata mafanikio zaidi kwa kupiga hatua kwenda kwenye timu kubwa zaidi ya uliyonayo. Benchi linaharibu mchezaji kisaikolojia.

2. Sina uhakika zaidi na malipo anayopata Kama yatakuwa ni sawasawa na yale malipo aliyokuwa akiyapokea pindi anasaini mkataba kwa mara ya kwanza. Pengine malipo anayoyapata ni kawaida tu kutokana na kutokuwa na mchango mkubwa katika timu japokuwa ana uhakika wa kulipwa mshahara wake.(sina uhakika na hilo la malipo tofauti na awali inaweza kuwa kweli au si kweli ila nimejaribu kuwaza tu)
Hili kama ni kweli maanake anaua kiwango chake huku malipo anayoyapata ni kawaida ili mradi tu asionekane kuchuja thamani kwa kwenda timu kama Mtibwa, Lipuli, Biashara, n.k

3. Maisha binafsi nje na mpira

Hili umelizungumzia lakini hatuna ushahidi, yawezekana kaamua kujiandaa maisha baada ya mpira au pengine ikawa wewe unamuwazia hivyo halafu kumbe yeye mwenyewe katulia tu hana habari. Kujiandaa kwa maisha baada ya mpira ni kwa kila mchezaji haijalishi unacheza timu gani au level ipi, huwezi kuishi kwa mpira miaka yote. Kuna kuumia, kustaafu, kuchuja kiwango, n.k
MPIRA NI KIPAJI NA NI AJIRA PIA, MCHEZAJI ANATEGEMEA VYOTE VIWILI VIMPE FURAHA KISIKOSEKANE HATA KIMOJA. (KUONESHA UWEZO WAKE + KUPATA MALIPO MAKUBWA KUTOKANA NA UWEZO WAKE ANAOUONESHA)
 
Kiwango cha Beno kabla ya kutua Simba kilikua kinaweza kumpeleka mbali kisoka na kumwingingizia fedha nyingi sana, Hakukosea kujiunga Simba kwa wakati ule tatizo kwasasa hapati nafasi na alikua na uwezo mkubwa kuliko Manura.
Anachotakiwa ni kutafuta timu itakayo mfanya aurudishe kiwango chake, Kipaji chake akikifanyia kazi fedha atakayo ingiza ni zaidi ya utajiri wa asset zote za Simba ambazo MO alisema hazi zidi bilioni tatu.
 
Atavuta mkwanja ndio, ila atasugua benchi kwa miaka miwili kipaji kitakufa.
Mwisho wa siku mkataba ukiisha anakosa timu anaanza kuzurura mtaani
Juma mahadhi, farouk shikalo( professional player huyu), paul boxer, hawa hamuwaoni ila simba ndio wanaonekana, !! Ushabiki ni tatizo ase
 
Nenda yanga ukawachambulie mkuu, simba itakupa presha na ushabiki maandazi huo!! Beno Kakolanya anawauma sana , emu pambaneni na timu yenu
 
Wachambuzi wengi wa hapa bongo akili zao tia maji tia maji , wapo kishabiki na upupu mwingi akilini!! Baada ya kupiga makelele mitandaoni kuwatisha watu na mapokezi ya watu fulani airport pale, mambo yameenda kinyume , walichotarajia tofauti na kilichopigiwa makelele, !! Kuna watu walikuwa majina yenye kutukuzwa , mara mtu na nusu, kelele kibao, matokeo yake ni zero uwanjani na kurukaruka!! Wanachofanya saivi ni kugeuka upande wa pili kuendelea na kampeni zao za kipopoma!!
Uzuri kampeni hii tushaijua muda!!
Saivi kocha mpya anatukuzwa like god vile, !! Najua muda sio mrefu watachemka tena na upopoma wao
 
Ukiandika jaribu ku Balance story yako...
Wakati unaongelea mfano wa David De Gea kwenda kuwa sub ya Alison unatakiwa utueleze pia Huyo kipa namba mbili wa Man U anaubora gani? Ni kipa namba moja wa taifa gani? Argentina na Spain kuna utofauti gani mkubwa kisoka? Mbona kipa namba moja wa Argentina amekubali kuwa kipa namba mbili kwa kipa wa Spain hapo Man U? Je anaua kiwango?
Usivutie story upande wako ili upate conclusion inayo favour hoja zako...
 
Weka Statistics kuonyesha kiwango cha Beno kilikua bora kuliko cha Manura...kinyume na hapo acha kutudanganya.
 
 
Mkuu..mtu kama ajibu alikua na njaa gani yanga..na alipewa unahodha...gadiel nae alikua na njaa gan.....basi tuseme yanga kuna njaa lakini je ilikua sawa kwa wao kwenda simba?..mtu kama ajibu au gadiel kwann wasingeenda hata azam ambako wangeweza kucheza kila wiki.
 
Hao wachambuzi kama wachambuzi kweli wakamshauri Ozil pale Arsenal kwanini anakaa benchi wakati ana uwezo wa kucheza timu kibao.
Wale wachezaji hamuwalipii kodi wala kuwalisha isitoshe ni watu wazima sijui nini kinamwasha
 
Mkuu sins uhakika kama team captain huwa analipwa kuliko wenzie...suala la njaa lilikua ni la timu nzima...wachezaji walikua wanadai..mfano Beno.,Dante umesahau mkasa wa Ngasa? wakati upande wa pili wamekufuata wanalipa vizuri na wamekuja na mkataba mnono pamoja na bonus...tusiwalaumu mkuu badala take tuwatie moyo..mchezaji aliyesemwa miaka nenda rudi "Said Ndemla " mbona sasa anaanza kupata nafasi na National timu anaitwa.
Kwa staili hiyo hata wakenya wamlaumu Kahata kwa kwenda Simba wakati Gormahia alikua anacheza?
Kuwa competent siyo kukimbia ubora wa kikosi ni kupambana hapohapo na kushikiria namba yako...mbona Zimbwe kaletewa sana watu pale Simba lakini anaongeza bidii...uwezo wa Zimbwe wa Leo siyo ule wa 2017 uliomfanya awe mchezaji bora wa ligi..tuwape moyo tu.
 
Kuna watu mna akili maji, hivi ujinga uliouandika wewe si tutafute mwanamke wako tumfedheheshe?
 
Weka Statistics kuonyesha kiwango cha Beno kilikua bora kuliko cha Manura...kinyume na hapo acha kutudanganya.
Beno alikua anaitwa timu ya Taifa akiwa Yanga, katika vitu vinavyo thaminiwa na vinavyo mrahisishia mchezaji kupata timu nje ya nchi pamoja na Mambo mengine ni kucheza timu ya Taifa hasa kwenye uu ukanda wetu wenye Ligi mbovu. Mchezaji yoyote anaye jitambua anayetokea kwenye Ligi yetu ambayo ushindani ni mdogo anatakiwa ahakikishe anafanya juhudi kucheza timu ya Taifa, au mashindano ya vilabu Afrika ili aonekane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…