Beno Kakolanya ampa makavu mchambuzi uchwara David Felician

Beno Kakolanya ampa makavu mchambuzi uchwara David Felician

Beno alikua anaitwa timu ya Taifa akiwa Yanga, katika vitu vinavyo thaminiwa na vinavyo mrahisishia mchezaji kupata timu nje ya nchi pamoja na Mambo mengine ni kucheza timu ya Taifa hasa kwenye uu ukanda wetu wenye Ligi mbovu. Mchezaji yoyote anaye jitambua anayetokea kwenye Ligi yetu ambayo ushindani ni mdogo anatakiwa ahakikishe anafanya juhudi kucheza timu ya Taifa, au mashindano ya vilabu Afrika ili aonekane.
Sawa mkuu...Beno alikua anaitwa timu ya taifa...Je hiyo hoja ina justify kwamba Kiwango cha Beno kilikua bora kuliko cha Manula? Je ni nani alikua kipa namba moja wa timu ya taifa wakati Beno anaitwa?
 
Huyu dogo me namjua kitambo kabla hata hajaanza kufanya kazi na Shaffih Dauda.

Ni shabiki wa Yanga na demu wake anaitwa Ela kadem flani kahaya nacho kashabiki ka yanga.
Beno alikuwa hana hata haja ya kumjibu Davi ni dada tu.

Sheria za JF zingekuwa zinaruhusu naweka picha ya kadem chake hapa mcheke sanaa
Anza kuweka picha yako.
 
Mwandishi kawasilisha anachokiamini, lakini binafsi niliyaona makosa ya wacjezaji 2. Beno na Gadiel. Mchaezaji aloyechemka zaidi ni Gadiel maana hakufikiria kabisa anakokwenda anakwenda kuwa nani? Matokeo yake kaacha nyumba yake kaenda kupanga. Beno ni miongoni mwa vipaji halisi vya kitanzania, Lakini ameua kipaji kwa kukosea kuchagua. Najua wazi na nilimsema kocha aliyekuwepo kwamba anakosa sifa moja kubwa ya kuwa "Mlezi", akamkataa mchezaji kwa kosa la kudai haki yake hata kama hakutumia njia sahihi za kistaarabu. Hata hivyo alichokifanya mchezaji ilikuwa kama kuunga juhudi ushabiki wa Simba na Yanga, akakubali kutumika kama chombo cha siasa za mpira. Hakujali yeye atakuwa nani Simba, akakubali kuwa mke wa pili. Tuwapende wachezaji wetu lakini wanapokosea tuwaambie ukweli. Leo De Gea anaweza kwenda Liverpool kuwa msaidizi wa Allison? Hatuoni wenzetu hata nafasi yake uwanjani inaweza kuwa sehemu ya mkataba wake.
Kwani Liverpool wakimtaka De Gea kwa Dau kubwa atakataa kisa kuna Allison?

Golikipa wa Arsenal Szczesny alienda Juventus yenye ushindani mkubwa golini Leo ndio number moja.
 
Shida ya wandishi na watangazaji wengi wa habari, ni kua ni watu wa matukio sio wafuatiliaji wa habari. Jana tu wakati mechi inaendelea Baraka mpenja alisema asubhi simba imecheza mechi dhidi ya simba B, Je, nani alikua golini? Ni kweli inawezekana wanamtazamo sawa lakini shida yao hawaandiki kuwasaidia ila wanaandika kuwagombanisha na wajiri wao. Nani amefanya uchanguzi wa kwa nini apangwi akaja na majibu ya moja kwa moja kutoka kwa kocha badala ya kuangalia nadharia zao tu.
Walifanya hivyo hata kwa Ndemla ili ahame timu, Shida uwa wanaogea sio kumsaidia mchezaji ila kumgombanisha na mwajiri wake
 
Mkuu sins uhakika kama team captain huwa analipwa kuliko wenzie...suala la njaa lilikua ni la timu nzima...wachezaji walikua wanadai..mfano Beno.,Dante umesahau mkasa wa Ngasa? wakati upande wa pili wamekufuata wanalipa vizuri na wamekuja na mkataba mnono pamoja na bonus...tusiwalaumu mkuu badala take tuwatie moyo..mchezaji aliyesemwa miaka nenda rudi "Said Ndemla " mbona sasa anaanza kupata nafasi na National timu anaitwa.
Kwa staili hiyo hata wakenya wamlaumu Kahata kwa kwenda Simba wakati Gormahia alikua anacheza?
Kuwa competent siyo kukimbia ubora wa kikosi ni kupambana hapohapo na kushikiria namba yako...mbona Zimbwe kaletewa sana watu pale Simba lakini anaongeza bidii...uwezo wa Zimbwe wa Leo siyo ule wa 2017 uliomfanya awe mchezaji bora wa ligi..tuwape moyo tu.
Umeongea vema mkuu, shida ya hawa wandishi uchwara wanatumia hiyo mianya kutaka kuwagombanisha na wajiri wao, hakuna anayeandika kiufundi au kutafuta sababu za kiufundi kutoka kwa benchi la ufundi ili waviandike viwajenge Wachezaji, zaidi ya kuandika ili kuwabomoa
 
Huyu dogo me namjua kitambo kabla hata hajaanza kufanya kazi na Shaffih Dauda.

Ni shabiki wa Yanga na demu wake anaitwa Ela kadem fulani kahaya nacho kashabiki ka yanga.
Beno alikuwa hana hata haja ya kumjibu Davi ni dada tu.

Sheria za JF zingekuwa zinaruhusu naweka picha ya kadem chake hapa mcheke sanaa
acha kuandika upupu wewe, mambo ya demu wake mara Shafii yanausikaje hapa.
 
Ao wachezaji ni wapumbavu, Kama wangekua wanajitambua wangeomba watolewe kwa mkopo ili wawe wanacheza, ukicheza marakwamara kiwango kina imarika na unaweza kuitwa timu ya Taifa, ukiwa timu ya Taifa na unacheza nafasiyako ya kupata timu nje ya nchi inakua kubwa sana. Kwasasa wanakaa bench na mpirawao unakufa. Ni Jambo la kuhuzunisha kipaji Kama Cha beno kinaoza, ana nafasi ya kufika mbali Kama akijitambua.
afike mbali zaidi ya hapo?
tumia akili basi mtu kama Kakolanya unataka awe kipa wa kimataifa na umri upi?
 
Aiseee ila Waswahili sisi tunajua sana kuwapangia wengine maisha yao.

1.Nianze ha huyo Mwandishi;yeye yuko tayari kuendelea kufanya kazi hapo kwenye kituo cha habari bila kulipwa mshahara na stahiki zake nyingine? Fedha kwake si kitu ilimradi anapata nafasi ya kuandika gazetini/kutangaza luningani na kusifiwa kwamba yeye ni Mwandishi mahiri? Ukisikia sifa za kijinga ndo kama hii sasa.

2.Hivi mnajua mipango ya Beno ni ipi? ndo maana ana hasira kwasababu mnajifanya mpo kichwani mwa mtu na mnajua mipango yake ya baadaye. Ni hivi:si kila mchezaji anataka namba kwenye first eleven au nafasi nyingi za kucheza, wengine wanataka mshahara tu ili uwasaidie kufanya future investment baada ya maisha ya soka, na pale Simba Beno anaenjoy mshahara mnono tu na kupitia huo ana miradi mingi tu anafanya kwa sasa, na baada ya miaka kadhaa itakuwa inamwingizia fedha ya kutosha.

Najua hutakubaliana na mimi katika hoja yangu namba 2 hapo [emoji121].Lakini ukweli ni kwamba kuna wachezaji leo wana-focus zaidi maisha ya baadaye kuliko sifa za kucheza kila siku na kuonekana kwenye first eleven. Kwani wangapi walikuwa wanacheza kila mechi ila leo ni hohehahe na ombaomba was kutupwa? Mpira ni pesa na malengo ya mbeleni huko. Hiyo nafasi ya kucheza huku hulipwi mshahara kaitumikie wewe.
ndiyondiyo
 
Sijawahi kuona Mchezaji Pro anawajibu wachambuzi,washabiki wa Simba na Yanga wengi hawatumii akili,imagine anasifiwa alichofanya ha ha
 
Kiwango cha Beno kabla ya kutua Simba kilikua kinaweza kumpeleka mbali kisoka na kumwingingizia fedha nyingi sana, Hakukosea kujiunga Simba kwa wakati ule tatizo kwasasa hapati nafasi na alikua na uwezo mkubwa kuliko Manura.
Anachotakiwa ni kutafuta timu itakayo mfanya aurudishe kiwango chake, Kipaji chake akikifanyia kazi fedha atakayo ingiza ni zaidi ya utajiri wa asset zote za Simba ambazo MO alisema hazi zidi bilioni tatu.
unaandika utopolo daah
 
Sababu ipo.
Kuna wachezaji wangapi wapo benchi mbona hawasemi?..
Beno Hana shida pale Simba ndo maana unamuona hachezi lakini halalamiki.
MAANA MSHAHARA WAKE ANAPATA.
Pale yanga alikuwa anacheza lakini mshahara wake alikuwa HAPATI NDO MAANA ALIKUWA ANALALAMIKA.
Beno anachoangalia mwisho wa mwezi mshahara wake uingie.
Kazi ya yeye KUCHEZA au kutokucheza anajua kocha hyo sio kazi ya Beno.
BENO YUKO SAHIHI.
Hapa Beno Kakolanya Kapanic pasipo sababu
 
Huyo mchambuzi kwanini asiende ndanda kumuhoji shiza kichuya aliyetoka misri akaangukia ndanda?
Sijawahi kuona Mchezaji Pro anawajibu wachambuzi,washabiki wa Simba na Yanga wengi hawatumii akili,imagine anasifiwa alichofanya ha ha
 
Back
Top Bottom