Beno Kakolanya aomba mkataba wake Yanga uvunjwe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa zinaonyesha kwamba Wanasheria wake tayari wamewasilisha ombi hilo kwa viongozi wa Yanga

Binafsi naunga mkono madai yake

========

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Samwel Lukumayi amesema wapo tayari kuachana na kipa wao Beno Kakolanya baada ya kukaa na wanasheria wao.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, alisema wamepokea barua ya mchezaji huyo akiwataka kuvunja mkataba nao.

"Kakolanya ametuandikia barua ya kutaka kuachana naye kwamba mkataba umevunjwa, tumeipokea barua hiyo na tunaipeleka kwa wanasheria wetu kuona itakavyokua," alisema Lukumayi.

Alisema fedha zake za mishahara tayari walishamlipa kama ambavyo wachezaji wengine walivyotakiwa kuzipata.

Aliongeza kwamba hawana kipingamizi cha kuzuia kuvunja mkataba wa mchezaji huyo kama wanasheria wataizinisha hivyo.

Kakolanya alikosekana katika kikosi hicho tangu mechi ya Yanga na Mwadui iliyofanyika mkoani Shinyanga kwa kushinikiza kudai fedha zake na ndipo kocha Mwinyi Zahera aliibuka na kusema kwamba hamuhitaji mchezaji huyo katika kikosi chake kutokana na utovu wa nidhamu.


Chanzo: Mwananchi
 
Kuvunjwa mkataba ni jambo la hiari kati za pande mojawapo, yeye avunje
 
Kwa nn unaunga mkono hoja yake

[emoji375][emoji375]
 
Kwa nn unaunga mkono hoja yake

[emoji375][emoji375]
ili asiue kiwango chake , maana ni kama hana timu na huku kiwango chake kikiwa juu kuliko kipa yoyote Tanzania
 
kwa sasa hakuna mwenye shida na mwenzie , yanga walishamtupa na yeye kawatupa
Huwa niko sawa kabisa nawe lakini waTz kwa tabia tuna uswahili sana. Na ndiyo maana wachezaji wetu wanashindwa kucheza michezo ya kulipwa. Tabia aliofanya Kakolanya haikubaliki kwa professional. Na Yanga nayo haikufanya mambo ki professional. Ndiyo maana nikasema tunasumbuliwa na unafki na uswahili .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama Zahera ni mganga huko kwao DRC lakini huu utakuwa zaidi ya uchawi
 
Ukiomba kuvunja mkataba wewe ndiye unayelipa gharama mlizokubaliana kwenye mkataba ikiwa itatokea kuna uhitaji huo. Refer Man Utd Vs Mourihno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…