Beno Kakolanya imeinajisi kazi yake

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Aaaa! Beno hasomi alama za nyakati, kazi yake ya ugolikipa ni kazi takatifu haitaki vitendo kama hivyo alivyofanya. Hii ni sawa na kuitia najisi kazi yake ya ugolikipa.

Hakuna timu makini duniani itapenda golikipa mwenye historia ya tabia kama hiyo ya kugoma anapokuwa na shida hasa ya kifedha. Hii inamaanisha kuwa golikipa kama Beno ana uwezo wa kuchukua fedha kutoka timu pinzani na kuiuza mechi ili kukidhi shida yake ya kifedha ambayo mwajiri ameshindwa kuiona au kuitimiza.

Aliyemshauri Beno kufanya hivyo alikosea sana kupita kiasi. Beno hataaminika pahala popote duniani kucheza kama golikipa, maana hawatajua akikasirishwa na uongozi atachukuwa hatua gani kama sehemu suluhisho ya shida yake.

Namshauri Beno aende Yanga akapige magoti kuomba msamaha kwa alichofanya ili kujisafisha. Yeye bado mdogo sana, anazo kesho nyingi sana ambazo zitahitaji umakini na trust ya hali ya juu wa wadau mbalimbali anaowafahamu na asiowafahamu.
 
Yanga tumeanza kukomaa kisaikolojia.
Tunapitia kipindi Kigum cha kukosa fedha ila tumekuwa atulivu sana tunafanya maamuzi taratibu hakuna ile migogoro na kelele kama misum iyo iliyo pita.
Dozi tunaendelea kugawa taratibu taratibu bila kelele
#Yanga Daima mbele
#Tim ya Wananchi
 
Uko sahihi....ila Yanga tumsamehe na tufanye tuwezavyo tumlipe tumalizane naye....umoja wa wachezaji na timu kwa ujumla ni muhimu sana wakati huu...nashauri atafute timu nyingine, tumtengeneze Kabwili na kumuamini, Aidha tutafute golikipa mwingine mwenye uzoefu na ligi kumpa changamoto Kabwili..."Yanga kwanza Maslahi ni Haki yatafwata."
 
Anashauriwa na meneja wake ambae ni mnazi na kiongozi wa Mikia FC.
 
Mlitaka acheze bure kama hamtaki kumlipa!
Hamna hela halafu bado mnamwona msaliti
Sasa timu iko ktk hali ngumu kifedha, Mashabiki na wapenzi wa soka wanajua, wachezaji, kocha n benchi la Ufundi wote wanafahamu, sasa ww Kipa ni nani ugome ktk mazingira haya ushinikize ulipwe, wakati hali unaijua....wachezaji wengine nao wakifuata mkumbo na kugoma kutakuwa na timu kweli....Binafsi pamoja na Dai lake la haki, nasema atafute timu nyingine akacheze....kuvuruga team spirit iliyopo Yanga sasa ni sawa na kuvuruga kazi nzuri inayofanywa na Kocha Zahera......aende hata Simba aende tu....
 
Kina Yondani na kessy waligoma baadaye kessy akaondoka,mlimwaminije Yondani halafu akaendelea na msimwamini Beno?
Mbona hamweleweki,sema mmeona labda mashahara wake ni mkubwa mnapotezea tu mda kama kessy then siku ya usijili unaisha mnampotezea tu na kumchinjia baharini,yeye kashasoma alama za nyakati
 
We Mika FC pambana na hali yako.
 
Mtatuelewa tu.......
 
Msemaji wa ndala mbumbumbu fc alishawahi kusema kama shida hizi zingekuwa upande wao yaani wangeshuka daraja lkn YANGA ni timu kubwa Africa inatatua changamoto zake kwa ustahilifu mkubwa mwaka Jana walifanya figisu sana yaani wiki moja tunacheza mechi tatu mfulululizo lkn bado tuliendelea kufanya yema

Leo kwetu

Sijui kesho kwa Nani

Yanga oyeeeeeeee

Nyuma mwiko
 
Tuwalipe wachezaji wote wanaoidai timu sio Beno tu. Ukimlipa Beno na kuwaacha wengine itaamsha maBeno wengine watakao tumia dawa ya Benoquine kutibu ugonjwa wao wa Yangalitis
 
TETESI: Inaelezwa kuna uwezekano katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo Simba ikamuacha golikipa wake Said Mohamed 'Nduda' ambaye anaonekana hana nafasi na nafasi yake ikazibwa na Beno Kakolanya.
Source: Shaffih Dauda IG

NB: Naona hapa ndio anaenda kuuwa kiwango chake
 
Yeye alishaaminiwa na timu kubwa kama Yanga kuwa kipa namba moja. Angekuwa mimi ningecheza kwa nguvu bila hata senti moja ili timu zenye hela ndani na nje ya nchi zinione. Ona wachezaji wenye akili kama Asante Kwasi alicheza kwa moyo wake wote Mbao FC hadi timu zenye hela kama Simba zikamuona na kumsajili.
 
Tuwalipe wachezaji wote wanaoidai timu sio Beno tu. Ukimlipa Beno na kuwaacha wengine itaamsha maBeno wengine watakao tumia dawa ya Benoquine kutibu ugonjwa wao wa Yangalitis
Ni sahihi, ndio maana nikasema tukiwa na uwezo wa kulipa wote ni vizuri...lkn kama hatuna uwezo huo Beno tukimlipa basi na akatafute timu nyingine.....na hata tukibahatika kuwalipa wote kwa wakati, pia Beno hastahili kuwa kikosini ili kuepuka huo ugonjwa kusambaa
 
Nafasi ya golikipa ni tofauti kabina na nafasi nyingine uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…