kaniki; sina experience na C Class.
Ila E Class naweza kusema ni gari Ngumu sana. utakumbuka zamani UwT na Ikulu walikuwa nazo nyingi tu.
Mfano mimi toka 2005 sijawahi kubadili Spares zozote hadi this month nilipojilazimisha kubadili Shock-Up, tyre rod ends, Ball joints n. ingawa bado gari ilikuwa inatembea.
At around 150,000 KM E series bado inapeta wala engine hiona dalili yoyote ya kuchoka. Ndo kwanza wakati mwingine engine inatoa hata mist ukiwasha gari asubuhi.
Spare parts zinapatikana Mpya na Used. Ukienda pale Mivinjeni Kilwa Road kuna mafundi wazuri sana tena kwa bei nzuri tu.
E series sasa hivi unaweza ukaiagiza japan kati ya $ 1500 hadi $ 5000. Ukinunua zaidi ya hapo, then umeliwa hauko makini kutafuta souce nzuri.
Mengine nisiongee kwa kuwa hujauliza. Ila kwa ufupi, kama umewahi kuendesha gari za namna tofauti 4WD au saloon za Class zote, bado utakubaliana na mimi hakuna gari yenye Confort kama Mercedez Benzi at least E Series ninayoijua mimi.