Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Bernadetha Kafuko, amesema Tanzania inahitaji kuwa na mifumo madhubuti ya mazungumzo na kuheshimu tofauti za kimtazamo, kisiasa na kimfumo, akisisitiza kuwa tofauti hizo zinapaswa kuonekana kama nguvu ya taifa na si udhaifu au uadui.
Kafuko amesema kutokana na mifumo ya demokrasia kutikiswa, tofauti za kimawazo zimeanza kuchukuliwa kama uadui, jambo ambalo si tafsiri sahihi ya demokrasia. Amesema tofauti za mawazo zinapaswa kuwa fursa ya kushawishiana kwa hoja na kufikia mwafaka, huku zikitumika kama chachu ya maendeleo ya taifa.
Amesema katika kutafuta mwafaka wa kitaifa, Katiba bora, utulivu na amani, ni muhimu kuwa na mazungumzo jumuishi na shirikishi yanayohusisha wananchi, taasisi za umma na wadau mbalimbali wa demokrasia.