RIP Super BM
Ngoja nitoe kisa kimoja cha BM ambacho sitakisahau,
Nakumbuka miaka ya Nyuma aliwahi kumwalika yule mmakonde mkuu wa nchi moja ya visiwani(Anjouan) wa wakati huo mwaliko binafsi kwenda kule kijijini kwao na kumuahidi kwamba kuna fursa kibao,
Hakutaka kuwashirikisha wenye mkoa, siku moja kabla ikabidi utaratibu ufuatwe , maana mkuu wa nchi hawez kufika kwenye mkoa bila wenye mkoa kushirikishwa kuandaa taratibu za kiprotokali, wakapewa taarifa
Kesho yake yule mkuu wa Visiwani akafika na dege lake binafsi akapewa ulinzi, sasa kiutaratibu wa wakati ule alitakiwa apande gari la mkuu wa mkoa, lakin BM akalazimisha bendera itolewe kule iwekwe kwenye gari lake na ndilo ambalo yule mkuu alitakiwa apande(kwa mujibu wake yeye)
Yule Mzee Mchaga mwenye mkoa wake akaamua kuondoka kurudi ofisini kwa ushauri wa mkuu wa usalama wa mkoa(yule mzee muislam kipara), then baadae yule mkuu na BM wakaenda kusaini kitabu cha wageni tayar kwenda kuoneshwa fursa na BM,
Siku ile nakumbuka kulikua na matope sana na kama mnavyojua ardhi ya kule tena, mara Paap Rais wa watu alikua kavaa Cobaz akateleza nusra apige kichwa chini walinzi imara wakaokoa jahazi,
Kufika kwenye fursa akaoneshwa nyumba ya ukoo(nafikiri ya mjomba) wake BM, akashawishiwa ainunue ili ajenge sehemu ile maana mbeleni kuna miradi mikubwa ingekuja pale,
Wasaidizi wa yule mkuu, kuiona nyumba yenyewe na eneo ilipo(Kijijini haswa) wakapatwa na hasira na kumwambia yule mkuu waondoke kwa kua pale hamna chochote,
bhas kwa huzuni BM akakosa mamilioni ya yule mkuu wa nchi ile,
Na ofcourse alifedheheka na kuaibika sana, akaamua kurud mjini Daslam kinyonge kabisa,
Mwamba alikua anajiamini sana, RIP Super BM