Bernard Kamilius Membe apokelewa kwa heshima kubwa CCM


Hii nchi inabidi tukubaliane Kama tunataka mfumo wa vyama vingi au la. Leo CCM wanafanya mkutano wa hadhara hawazuiliwi lakini Juzi CHADEMA wamezuiliwa kisa T-shirt zao.
 

Ndio mkiambiwa upinzani sio lelemama muelewe. Membe alikosa ushawishi upinzani Bora amerudi CCM . Upinzani hakumfai mwanaccm aliyekulia huko. Upinzani ni kwaajili ya wabishi akina Tundu Lissu waliopigwa risasi lakini hawakuhama. Membe kubebewa pesa zake kakubali kurudi CCM . Respect kwa Viongozi wa upinzani wenye msimamo hasa CHADEMA.
 
Naona ametoka kwenye tawi la ccm (ACT) na kurudi makao makuu

 
Mbowe kalelewa wapi?
 
Hii nchi inabidi tukubaliane Kama tunataka mfumo wa vyama vingi au la. Leo CCM wanafanya mkutano wa hadhara hawazuiliwi lakini Juzi CHADEMA wamezuiliwa kisa T-shirt zao.
Kwani wakubwa wa Chadema mbona huwa wanakwenda Ikulu kuongea na Mkuu huwa wanasahau kumweleza habari hii ya kuzuiliwa ??!!!
 

Kapokelewa karibu na Mbuyu, Sio kwa hehsima
 
“Sababu ambazo zilinifanya niondoke CCM haziko tena, narudi sababu zilizoniondoa CCM haziko tena. Nimerudi, namshukuru Mwenyekiti wa CCM na wajumbe wa Kamati Kuu kunirudisha”

Niguse ninuke.!!
 
Hivi bado ana ndoto za urais huyu Membe? au ndiyo wanamtayarisha Nape, nchi hii haitaisha vituko na ujinga!
 
Ila huyu mwamba hana mvuto kabisa kisiasa.😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…