Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Hata wewe katiba ya nchi inakupa haki ya kuchagua na kuchaguliwa,sasa kosa lipo wapi hapo? Mpeleke kwenye sanduku la kura ukamshinde huko.

Yesu wa Lugola na team yake wamewakaririsha utopolo tu.
Wewe ni mkwewe?
 
Maalim anavyomuangalia kama anasema "Wewe hutatuLowassa kweli?"
 
Kiukweli kabisa nimemsikiliza ma kuona upinzani wamepata kitu. Yuko tofauti labisa na lowasa, ana nguvu anatetetea hoja zake ila tatizo bad timing...ingekua ni 2025 amgelua na chansi maana iwanja uko wazi ila kwa sasa ni bad timing...hatoshinda ila amgalau kawachangamsha upinzani
 
Act wazarendo mmechemsha sana, hamjajifunza kilichowapata Chadema mwaka 2015? Mtakuwa kichekesho tu
 
Suala la mishahara ya vyombo vya usalama litapewa kipaumbele...mzee Membe unamaanisha nini?

Anamaanisha yupo pamoja na vyombo vya usalama na majeshi na wala hashindani hao Bali anashindana na Maghfuli na CCM yake.

Vyombo vya usalama lindeni nchi acheni CCM ipambane na vyama vingine kisiasa na ACT ikishinda maslahi yenu yataboreshwa.
 
Naona jamaa akiwatumia mabeberu kupata support. Uzoefu wake katika anga za kimataifa yaweza kuwa mtaji kwenye kufanya ushawishi.
 
Hahaha Mkuu unajua amekulia huko maisha yake yote. Mpaka asahau itachukua muda. Muhimu ni kwamba pole nyingi kwa wapinzani.
 
Mkuu kuna fumbo kubwa mno. Hawa watu wako kazini mpaka waingie kaburini. Kama aliachwa mpaka muda huu hakufanyiziwa jua yuko kazini. Kule ukienda vibaya kidogo kwa kudhamiria hutemi mate. Muda utasema
 
Hahahaaaaa. Hawa wapinzai ubongo wao umechanganyika mafuta ya taa.

2015 Mbowe alimpokea Lowasa, 2020 Zitto amempokea Membe!!
 
Mkuu kuna fumbo kubwa mno. Hawa watu wako kazini mpaka waingie kaburini. Kama aliachwa mpaka muda huu hakufanyiziwa jua yuko kazini. Kule ukienda vibaya kidogo kwa kudhamiria hutemi mate. Muda utasema
Chief wewe mbona hujatangaza nia? Magogoni pako wazi Jiwe amehamia Dodoma.
 
Ninekubaliana yote kasoro kumi.
Hii dhana ya kuuza malighafi nje ya nchi ndo inatufanya maskini.
Shughuli za kupandisha thamani mazao kama vile kubadilisha pamba kuwa nguo au mawese kuwa mafuta, zinathamani mara nyingi kwa taifa kuliko kuuza malighafi.
Tuache fikira za mkoloni na tuwe na mbinu za kweli za kuondoa umaskini.
 
Usiwe too emotional kila mmoja ana haki ya kuchagua na kutazama mambo kutokana na perspective angle aliyosimama. To me Membe yuko too ambitious na amekuwa blinded na ambitions.. Basi!

Membe kafukuzwa huko CCM na kahamia ACT kuungana to ambitious wenzie Maalimu Seif na Zitto.
 
Si mbaya kumpokea ila msimuweke kama lowasa acheni Tundu apiganie kiti cha urais kupitia vyama pinzani alafu Membe awe waziri wa ulinzi
 
Membe kafukuzwa huko CCM na kahamia ACT kuungana to ambitious wenzie Maalimu Seif na Zitto.
Binafsi naamini kila mara mahali pa kazi ni lazima pawe na figisu figisu hivyo dawa ya tatizo si kukimbia maana ukikimbia Tatizo unazidisha ufa.
Mwinyi asingekuwa mvumilivu wakati ule alipolazimika kujiuzulu Mambo ya ndani kwa sababu ya kiuwajibikaji leo hii CV yake ingekuwa tofauti.
Kikwete naye mzunguko wake ni mrefu ilia uvumilivu wake ulimfikisha alipo.
Magu as well, muhimu ni kuwa na msimamo na kutoyumbishwa...
 
Membe sio mjinga,ana lake jambo,hakufukuzwa CCM kwa bahati mbaya,bali alitengeneza mazingira ya kutovumiliwa na wahasimu wake hadi wakamtema.
Tunachojua alitutangazia bila kivicho kuwa chochote chaweza kutokea toka June hadi October sasa ni July.
Sitashangaa akigeuka kipande kidogo cha baruti kitumikacho kupasua miamba mikubwa.Usimdharau mtu asieonekana kuwa na hofu unless unajua plan zake.
 
I dont trust politicians......AT ALL!
 

Hakukimbia kama Lowasa na Sumaye Bali amefukuzwa uanachama kwa kudhililishwa na akina Magufuli,Bashiru na Polepole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…