Nilipokuwa nasoma shule ya bweni A level, kuna jamaa alikuwa akilazimisha sana awekwe kwenye timu ya shule kwenda UMISETA.
Hiyo ni kwasababu alijiona ni maarufu kwa jina lake na alipenda sana kusifiwa.
Alifikia kufanya shopping ya vifaa vya michezo na akawa amejiandaa kwelikweli.
Alilobby huku na kule kwa mwalimu wa michezo na walimu wengine wakawa wanamuonyesha wanamuonea huruma, lakini kumbe walikuwa wakimwangalia tu akihangaika.
Jamaa alikuwa na tabia ya kukosa maadili ikiwemo tabia ya kutoroka kwenda vijijini kupata ulabu.
Lakini siku wachezaji wote wanapanda basi la kwenda kwenye UMISETA yalipotajwa majina yote kwenye orodha jina la jamaa halikutajwa na akawa "very disappointed".
Michezo ya UMISETA ilipokwisha alijikuta anakubali ukweli kwamba hakustahili kwenda huko.
Nimeishasema humu mara nyingi kwamba kiufundi na kimfumo haiwezekani kwa Bernard Membe kuwa raisi wa nchi hii.
Na hali hiyo inazidi kujidhihirisha.