Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Kuna mmoja alisema ccm sio baba yake wala mama yake leo analamba miguu ya jiwe
 
Yaani achana hata na Lowassa huko mbali

Mimi kila nikimuangalia A. Kinana kwa jinsi alikua well connected na ushawish wake ndani ya chama na amerudisha mpira golini

Nabaki nawahurumia tu "wafuasi" wa ACT kwasababu Zitto na Membe sio watakaopoteza hawa wawili wanajua wanachokifanya na wanajua kabisa hawana ubavu wa kushindana na Chuma.

Wanavuta muda tu watarudi " To kiss pope's ring"

Halafu eti kuna Watanzania tena wanaojiita ' Great Thinkers ' wanaamini Membe na ACT-Wazalendo yake ina Ubavu kwa Rais JPM na CCM yake.
 
Ila kweli hata mbunge mmoja wanaweza wasimpate kama Zitto hagombei,hata akigombea naona wazi uchaguzi huu CCM watatumia mabavu kupora majimbo yote
Naona umeona Aibu tu Kuwachana ' Live ' Mkuu ni kwamba ACT-Wazalendo hawatopata hata Mbunge Mmoja na Membe ' ataangushwa ' vibaya.
 
CCM ni ILE ILE. ACT na vyama vingine vya upinzani havina focus ya nini wanahitaji.

Wamekuwa wachezaji wa ngoma ya CCM na waitikiaji wa pambio zao.
 
Tatizo huyu Bwana Membe anajiona Nyangumi kuuuuumbe yeye ni Dagaaa tu, naaamini wafuasi wake hawamwambii ukweli ili waendelee kupiga mpunga wake. Ndugu yangu Membe Umaarufu wako unaishia hapo Chalinze na huko kwenu Lindi vinginevyo labda unachofanya ni Maigizo tu.

Acha tu Mkuu ' Wajanja ' wampige Pesa zake zile za Gaddafi na Yule Balozi ( aliyekufa Kiutatanishi ) Ubalozini DSM ila ni ' Mwepesi ' kama Tissue.
 
Pole sana mzee Membe, siasa ngumu, hadi sasa hujanivutia tangu umeanza kuongea, hujatoa hoja badala yake unalalamika ya akina Sanane na Azori, tushawishi tukupe kura mzee.Bora tumsikilize Seif, halafu anaongelea magogoni, wakati tuko chamwino
Eti hakutakuwa na kutumbuliwa
Huyu membe mzima kweli?
 
Kumfananisha Membe na Maalim Seif ni first class mistake. Membe alifukuzwa CCM kutokana na tamaa yake ya kutaka kuwa Rais pamoja na chama kuwa na tamaduni zao za siku nyingi (huu sio msimamo kama wa Maalim)

Maalimu Seif alifukuzwa kwa tuhuma za kuutaka uraisi wa Zanzibar na msimamo wake wa Serikali tatu. Utakuwa umezaliwa juzi na wala hufuatilii dulu za kisiasa za nchi hii au wewe Mnywaranda.
 
Nilipokuwa nasoma shule ya bweni A level, kuna jamaa alikuwa akilazimisha sana awekwe kwenye timu ya shule kwenda UMISETA.

Hiyo ni kwasababu alijiona ni maarufu kwa jina lake na alipenda sana kusifiwa.

Alifikia kufanya shopping ya vifaa vya michezo na akawa amejiandaa kwelikweli.

Alilobby huku na kule kwa mwalimu wa michezo na walimu wengine wakawa wanamuonyesha wanamuonea huruma, lakini kumbe walikuwa wakimwangalia tu akihangaika.

Jamaa alikuwa na tabia ya kukosa maadili ikiwemo tabia ya kutoroka kwenda vijijini kupata ulabu.

Lakini siku wachezaji wote wanapanda basi la kwenda kwenye UMISETA yalipotajwa majina yote kwenye orodha jina la jamaa halikutajwa na akawa "very disappointed".

Michezo ya UMISETA ilipokwisha alijikuta anakubali ukweli kwamba hakustahili kwenda huko.

Nimeishasema humu mara nyingi kwamba kiufundi na kimfumo haiwezekani kwa Bernard Membe kuwa raisi wa nchi hii.

Na hali hiyo inazidi kujidhihirisha.
 
Halafu Jamaa mwili wake unakibaridi utadhani ni mtu anayesimamia samaki na kutoa samaki kwenye majokofu pale bandarini Kwa ajiri ya kuwauzia wateja wa madale, kumbe ni jasusi wa ACT
 
Lowassa alijitoa CCM kwenda kujaribu bahati ya urais. Kilichompeleka upinzani ni TAMAAM YA URAIS.

Membe AMEFUKUZWA CCM sababu ya kudai haki za kikatiba. Kinachompeleka upinzani SIO URAIS bali ni kutafuta HAKI.

Kwa vyovyote vile naona hesabu haziko upande wa Membe

Kuna swali nimekua najiuliza toka hizi harakati zake za kwenda ACT zianze. Hivi kwanini hakuondoka 2015 na Lowassa aje aimarishe huo upinzani halaf Lowassa agombee uRais

Mbona aliacha miaka 5 yote mpinzani wake ajisimike vizuri chama/dola??

Majibu ni mawili tu 1:Hana nia ya dhati na 2:Sio strategist mzuri

Na majibu yote hayo manaake ni moja tu. Hafai
 
Acha tu Mkuu ' Wajanja ' wampige Pesa zake zile za Gaddafi na Yule Balozi ( aliyekufa Kiutatanishi ) Ubalozini DSM ila ni ' Mwepesi ' kama Tissue.
Hahahaaaaa, kipindi hiki wapo Vijana wajanja ndani ya Chama wanaanzisha mpaka miradi mikuuuuubwaa kwa pesa za watu dizaini hii.
 
Back
Top Bottom