Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Nilidhani atakuja na mafuriko leo
Au ndo wanasubiri CCM iwatema wengine
 
Kila la kheri BM katika kusaka demokrasia ya kweli,jiandae na mabomu huku
 
Mafisi kazini!
 
Hotuba nzima sijaona akizungumzia kuungana.

Terms and conditions zimegonga mwamba au till further notice.
 
ACT Wazalendo,

Hivi CCM yangu nao hawana Verified Account yao hapa Jamvini JamiiForums? Kama hawana 'wananiangusha' mno na ninaomba wawe nayo pia.

Kwa kweli CCM wako nyuma sana katika Nyanja ya Mitandao za Kijamii hapa tuna TLP Taifa , ACT Wazalendo pamoja na CUF Habari . Wajifunze na wabadilike!
 
Amejiunga ACT kujaribu bahati yake na kukidhi kiu yake ya kugombea urais. Zitto yeye mahesabu yake ni ongezeko la ruzuku kwani anajua fika Membe hawezi shinda urais ila kura atakazopata zitaboost ruzuku.
Ahadi ambazo Membe ametoa anajua wazi ni uongo mtupu. ACT haiwezi kuajiri wahitimu wote wa vyuo vikuu, hawawezi kuongeza mishahara kiasi wanachojinasibu labda kama wanataka kuchochea inflation.
Msimu wa uchaguzi huu watu wanadanganywa sana.
 
2015 Kwa cdm ya Lowassa ilikuwa fundisho tosha. Kwenye hili la Membe kwenda ACT, muda utakuwa mwalimu mzuri.
Labda ingeeleweka "fundisho" lilikuwa vipi, maanake kuna kuwa na uelewa tofauti.

Kwa mfano, uelewa wangu kuhusu Lowassa na CHADEMA huenda ni tofauti na wako.

Mimi nilivyoelewa ni kuwa Lowassa alikuwa anatafuta u-Rais kwa njia yoyote ambayo ingemwezesha kufanya hivyo. Baada ya kuukosa CCM, akaona njia iliyopo ni kupitia CHADEMA.

CHADEMA, wao walidhani kwa kumkaribisha Lowassa, ambaye kimwonekano alionekana kuwa na wafuasi wengi, ingekuwa ndio njia ya kushika serikali, kupata wabunge wengi.

Pande zote mbili hawakufanikiwa kufikia malengo yao.

Nisichoweza kujibu hapa ni kama malengo hayo yalikuwa ni kwa manufaa ya wananchi, au kwa manufaa ya wenye malengo. Lakini hili nalo linaweza kujadilika.

Kurejea kwa Lowassa CCM na kukupa aina fulani ya tafsiri ni kukosa umakini, kwani ni dhahiri kwamba kapoteza mengi.
 
Hiki chama chenu hata hakieleweki, hivi kati ya Mwenyekiti wa chama na Kiongozi wa chama ni nani mwenye nguvu ndani ya chama! Nani anampagia mwenzie majukumu? Na Membe atakuwa na cheo gn? Dah kizunguzungu tu
Zitto kajimilikisha chama chote, Hizo nafasi zingine za uongozi ni geresha tu, Hio nafasi ya kiongozi mkuu haigombewi ni ya milele
 
Hiki chama chenu hata hakieleweki, hivi kati ya Mwenyekiti wa chama na Kiongozi wa chama ni nani mwenye nguvu ndani ya chama! Nani anampagia mwenzie majukumu? Na Membe atakuwa na cheo gn? Dah kizunguzungu tu
Swali hili aulizwe Prof. Kitila Mkumbo aliyeshiriki kuanzisha na kuandika Katiba ya Chama hiki cha ACT-Wazalendo.
 
Mbona hata sasa ipo hivyo hivyo? Uliza kina Mwigulu, Simbachawene etc.
 
Hongera kwetu kwan membe analeta changamoto kwenye siasa yetu
Kuhusu uchaguzi kwangu hapana lkn namkubali na tz itamuhitaji baada ya 2020
 
Daaaah yale yale, ebu tuone NCCR kama watafanya upuuzi kama huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…