Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

ACT Wazalendo tukiingia Ikulu October 2020.


1. Tutashughulikia kwa ukamilifu tatizo la ajira kwa vijana na wale wahitimu wa vyuo vikuu ambao wapo vijiweni bila kazi.

AHADI HII NDIYO MLIYOINGIA NAYO WEWE NA NDUGU YAKO DR. KIKWETE NA MKAGUNDUA KWAMBA NI MANENO MATAMU KWABAJILI YA KUWAKUSANYA MAJINGA

Kwanini msiseme mtabadilisha mfumo wa Elimu ili uwe wezeshe katika kujiajiri kuliko kulundika ma academician mtaani?

Hujagundua kwamba tatizo sio Rais aliyepo madarakani bali mfumo wa Elimu?

**************

2. Swala la mishahara ya watumishi wa vyombo vya usalama litapata kipaumbele.

Tutapandisha mishahara ya wafanyakazi wote ambao kwa kipindi chote cha miaka mitano hawajapata nyongeza za mishahara na promotion.

FIRST THING FIRST

Naona UMEAMUA kuwa - blackmail wana, kwanza hii ni ishara mbaya sana kwa mtu ambaye tunategemea awe wetu na sio Rais wa kundi fulani

**************

11. Bagamoyo Port expansion itapewa kipaumbele.

Despite of the facts alizotoa Mkuu mzee baba unataka Urais ili ututie sokoni tena?

************

13.Bureu du Change zote tutazirudisha na madai yote halali ya wafanyabiashara wa maduka ya kubadilisha fedha yatashughulikiwa na kulipwa.

HATA KAMA WALIKUA WALIKUA WANA SABOTAGE UCHUMI WA NCHI?

MWISHO JAPO SI KWA UMUHIMU
Sijakusikia ukizungumzia RUSHWA mzee au yenyewe haikukeri kabisa? Vipi kuhusu haki za wanawake na Watoto wa kike mashuleni?


MAJUMUISHO YANGU
Ndege mmoja aliye mkononi anathamani kuliko wawili walioko mtini.

Ahsante kwa kujaribu.
 
Hukutakuwa na hofu ya kutekwa, kutumbuliwa wala hofu ya kupoteza uhai kwenye utawala wetu.
Hotuba nzuri lakini hapo kwenye watu kutokuwa na hofu ya kutumbuliwa anatuma ujumbe gani?

Anamaanisha ACT mkishika dola basi watu wakivurunda, wakifanya matumizi mabaya ya rasilimali za umma, wakienda kinyume na maadili hawatawajibishwa?

Au kuwajibishwa kutakuwa kama mtindo ule wa zamani unaamishwa tu kituo cha kazi uende ukaharibu mahala pengine?
Naona huu mchezo unaanza hata kufanywa na serikali hii ya awamu ya tano, mtu anatumbuliwa kwa madai ameharibu sehemu kisha baada ya muda anaenda kupewa sehemu nyingine (Mfano: Mwigulu), ina maana hawa walisingiziwa au walitumbuliwa kimakosa?

Wanasiasa bwana wote kama mapacha wanaoshabihiana (identical twins).
Bora ubaki na zimwi likujualo halikuli likakumaliza, Mimi nabaki na Magufuli sababu nimeshamjua udhaifu wake na uzuri wake, he does more good things than harm to us.
 
Kwahiyo mnaiga ya dodoma? Cha ajabu zito kesho anaweza kuhojiwa dw na kusema watu wanakufa sana kwa corona na corona ipo kila kona

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
"Endelea kuchukua tahadhari" hii ni kauli ya kiongozi wangu wa nchi na ninaiamini kuliko unayosema wewe mkuu.
 
13.Bureu du Change zote tutazirudisha na madai yote halali ya wafanyabiashara wa maduka ya kubadilisha fedha yatashughulikiwa na kulipwa.
Hapa heko ACT, kuna minong'ono ya manung'uniko mengi huku mitaani.
Watu wapewe chao wakajaribu biashara zingine kama kweli wanadai chochote.
 
Izo kura zina simamiwa na tume huru!
hili ni swali la muhimu kwa wapiga kura wajiulize hivi kweli membe ana nia ya dhati kwenye uchaguzi huu bila kuwa na tume huru? wakipata jibu waamue na wachanganye na za kwao ndipo watamjua membe na wenzie wanaojiita wapinzani
 
Let them try what they can jaman, Sasa mnataka wamsimamishe Nani? Kuna wakati kufanya usajiri ni better
Kweli kabisa ccm chama dume , wagombea urais lazima watoke ccm.
 
Anatuambia atafufua Kikwete's agenda...

-Kuuzia Wachina Bandari Bagamoyo
-Kurudisha Bureau De Change
-Kurudisha waarabu/wahindi/wayemeni waliokimbia nchi
-Kufungulia jela kina Seth na mhindi wa Bank M ( sijui bado yuko ndani?)
-Kuacha kuwatingisha na kuwadhibiti wafanyabiashara na kuwaweka kitumbo joto kina Subhash Patel, Rostam Aziz, GSM, ACCACIA, na ile kampuni ilyokuwa inahodhi haki ya kuchimba Tanzanite....

MEMBE unajuaje hivi vitu ni popular kwa Watanzania? Umefanya wapi hiyo survey?

Hata ilani ya uchaguzi ya Shehe Ponda is more in tune with the priorities of the people
 
Dodoma hawaamini katika Barakoa, wameshaliweka wazi hilo.

Zitto amepigia kelele suala la barakoa na pandemic precautions kwa ujumla.

Ndo maana hapo watu wanawashangaa wanapokusanyika wao wenyewe hakuna barakoa!
Unaweza fikiri watu wanatetea maslahi ya wananchi kumbe wanatetea yao , ndio kama hivyo.
 
CCM ni wahuni sana. Wamekosa ustaarabu. Channel imekuwa hacked halafu inatumia kutangaza hotuba ya Kabudi UN! Huu ni uhuni wa hali ya juu. Kwa nini CCM hampendi ushindani wa kistaarabu?
 
Narudia tena, tofauti ya Lowassa na Membe, mmoja anapaka nywele picko, na mwingine kaachia mvi zionekane. Membe hakufukuzwa ccm, bali aligoma kuomba msamaha, kisha akazira na kurudisha kadi ya ccm. Katika mazingira hayo akaiacha ccm bila uchaguzi zaidi ya wao kuhitimisha kwa kutangaza kumfukuza.
Membe alifukuzwa CCM.
 
ACT Wazalendo,

Hivi CCM yangu nao hawana Verified Account yao hapa Jamvini JamiiForums? Kama hawana 'wananiangusha' mno na ninaomba wawe nayo pia.

Kimsingi ccm mambo mengi wanaiga kwa vyama vya kisasa. Haya mambo digital hawana jinsi, inabidi nyinyi wanaccm mnaoelewa haya mambo muwasaidie, maana wengi wao ni wazee, au kama ni vijana, basi ni wale wenye mitazamo ya kizee.
 
CCM ni wahuni sana. Wamekosa ustaarabu. Channel imekuwa hacked halafu inatumia kutangaza hotuba ya Kabudi UN! Huu ni uhuni wa hali ya juu. Kwa nini CCM hampendi ushindani wa kistaarabu?

Hawajawahi kuwa wastaarabu.
 
Back
Top Bottom