Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

2015 Kwa cdm ya Lowassa ilikuwa fundisho tosha. Kwenye hili la Membe kwenda ACT, muda utakuwa mwalimu mzuri.

Let them try what they can jaman, Sasa mnataka wamsimamishe Nani? Kuna wakati kufanya usajiri ni better
 
Narudia tena, tofauti ya Lowassa na Membe, mmoja anapaka nywele picko, na mwingine kaachia mvi zionekane. Membe hakufukuzwa ccm, bali aligoma kuomba msamaha, kisha akazira na kurudisha kadi ya ccm. Katika mazingira hayo akaiacha ccm bila uchaguzi zaidi ya wao kuhitimisha kwa kutangaza kumfukuza.

Tumetangaziwa Mara nne kwamba Membe amekufuzwa ndani ya CCM. Hiyo kukataa kuomba msamaha kwa kusimamia anachokiamini ndiyo kumemfanya afukuzwe uanachana.
 
Ujanja wote wa chama chako cha CCM ni kule mtaani tu kwa Watanzania "Wanyonge". Kwenye mitandao mfano humu Jamii Forums, wanaogopa bila shaka kutokana na madudu yao wanayotufanyia Watanzania.
CCM tunajielewa wewe .Wapiga kura wetu hawako mitandaoni wako mitaani na vijijini.Ndio maana hata midahalo mnayotaka ya wagombea uraisi huwa hatuitaki sababu wapiga kura wetu sisi wengi hawana TV.HATUWEZI UZA SURA kwa wenye TV ambao hawafiki hata asilmia tano ya wapiga kura !!!

Na watanzania wa kawaida hata awe na TV hujiaangalilia movie sio mambo ya siasa.CCM hatuwezi poteza muda kuuza sura kwa wenye TV majumbani kwanza wengi hata kupiga kura huwa hawaendi wanakaa nyumbani wanafuatilia tu kwenye TV

Mitandaoni wapiga kura hamna wako wachache sana
 
Hiki chama chenu hata hakieleweki, hivi kati ya Mwenyekiti wa chama na Kiongozi wa chama ni nani mwenye nguvu ndani ya chama! Nani anampagia mwenzie majukumu? Na Membe atakuwa na cheo gn? Dah kizunguzungu tu
Kwa Iran ni kama vile Supreme Leader 'AYATTOLAH 'vs Rais wa nchi.

So hapo Ayatollah ndio baba a lao.
 
Membe kaishukuru kamati kuu ya CHADEMA kwa kumpokea baadaye akasema ohh sio nashukuru kamati kuu ya ACT wazalendo!! Anaonyesha keshaongea na kamati kuu ya Chadema na wameshakubaliana sidhani kama kateleza ulimi hapana !!

WAZALENDO na CHADEMA wanaenda kuungana mgombea wao ndio huyu Membe mark my words ndio maana wajumbe wa kamati kuu waliotia nia kugombea chadema wa ndani akina Mbowe wamekimbia ugombea uraisi kiaina!!! kumpisha
 
Kumfananisha Membe na Lowasa/Sumaye/Nyalandu si sawa, Membe mfananishe na Maalim Seif maana wamefukuzwa uanachama ndani ya CCM kutokana na misimamo yao.
Hio kufukuzwa ni gia/story/sababu tu zimetafutwa za nitoke kwa style gani huku Ccm ili nijitofautishe na Lowassa?Jibu likawa hilo style ya kufukuzwa.

Membe ni mharibifu kama Lowassa tu akimaliza kilichompeleka ACT atarudi zake kwao CCM.
 
CCM wazee wa siasa chafu.

Baada ya lile bomu la 2015, naona sasa wamepanga kwenda kuharibu siasa ya wazalendo ya kina Zitto.
 
Back
Top Bottom