Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Umepewa macho lakini huoni, umepewa masikio lakini husikii na umepewa akili lakini huzitumii.Huyu jamaa, ‘jasusi mbobezi’, hana kabisa mvuto akiwa jukwaani.
Siasa kwake naona si jambo alilonalo kiasili.
Anajitahidi sana kuongea na kudondosha vibwagizo akiwa jukwaani, lakini wapi! Hamna kitu kabisa.
Maneno hayamtoki mdomoni kiulaini. Linganisha Lissu akiwa jukwaani na huyo Membe, ni usiku na mchana.
Sauti haina mvuto. Hana msamiati wa kutosha wa kuchotea vibwagizo kuendana na hadhira iliyo mbele yake.
Anachokiweza ni vijembe vya kimafumbo huko Twitter.
Kwa mwaka huu ccm lazima hesabuni vidonda tu na mjiandae kugombea KUB na akina NCCR na TLP na CUF ya Lipumba