Bernard Membe huna sifa wala uwezo wa kuwa 'campaign manager' wa Rais Samia

Bernard Membe huna sifa wala uwezo wa kuwa 'campaign manager' wa Rais Samia

U
Mkuu naona unaanza kusahau mapema, ebu kumbuka enzi za hayati Dr John Pombe Magufuli akiwa waziri wa ujenzi!
Umenikumbusha mbali sana.
JPM akiwa Waziri wa Ujenzi alishikamana sana na TANROADS, kiasi kwamba alipopata Urais, Tanroads ukawa MHIMILI wa NNE wa Utawala.
Vyombo vya Habari, ambavyo katika Nchi zenye Demokrasia huwa Mhimili wa Nne, vikawatupwa pembeni kwa kunyanyaswa?
Rushwa ndani ya Tanroads, ambayo matokeo yake ni ujenzi wa Barabara zilizo CHINI YA VIWANGO, ilihalalishwa.
Hata CAG aliteuliwa kutoka Tanroads.
DG Bandari alitoka Tanroads.
DG Viwanja vya Ndege toka Tanroads.
Msimamizi Mkuu Bwawa la Nyerere toka Tanroads.
Mshauri Mkuu ujenzi SGR toka Tanroads!
Hakika, Tanroads iligeuka Mhimili wa NNE wa Taifa.
Na haikuwahi kukaguliwa na CAG.
Hakika, umenikumbusha mbali
 
Bongo bwana, umaarufu alionao mtu mitandaoni nitofauti kabisa na uhalisia kwa wananchi wa kawaida(ambao kimsingi ndio wapiga kura)
 
Ujinga unaanzia kwenye kufikiria majina ya watu badala ya dira ya taifa na maendeleo ya watu! Natamani ifikie hatua mwenye maono makini ya kutuvusha apewe nchi aoingoze hata kama ni mgombea Binafsi!

Tumerudi nyuma sana! Tuamke!
 
Eti jasusi mbobevuuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].ukute ezekiel kamwaga akimsifuu sasaaa . utadhani ni bonge la jasusiii
 
Tokea Magufuli afe kuna watu wamekuwa wakiangaika kila kukicha nafikiri hawa ni wale waliokuwa wakinufaika na utawala ule wa kidhalimu na kikatili.
 
Nchi yetu inavituko sana, huyu ni kituko mwingine!!


Ila jamaa alitisha sana, eti kampeni hapigi halafu akasema ushindi ni asubhi tu na akasubiria dk za mwisho hahahhhhha wanasiasa wa bongoland /Africa vituko tupu
Eti ametenga 10b za kampeni[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aliyekuwa mgombea urais wa ACT Wazalendo kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 na akaishia kufanya kampeni kwenye kijiji cha Rondo huku akijinasibu kuwa anataingia na kufunga goli dakika ya 90 bwana Bernard Membe, leo mbele ya waziri mkuu ametangaza kumuunga mkono rais Samia na kusema yupo tayari kuwa kampeni meneja wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.!
Bwana Membe huwa anapenda kujitwisha sifa ambazo hana ,ikumbukwe mwaka 2015 aliingia tano bora kwenye mchujo na kuishia kubwagwa hadi na kijana mdogo January Makamba!
Bwana Membe amekuwa waziri kwa miaka 15 lakini hakuna alichoifanyia nchi hii na wala hana legacy yoyote aliyowachia watanzania


Membe asema yuko tayari kurudi mahali fulani | Mwananchi - Membe asema yuko tayari kurudi mahali fulani
Na asithubutu hiyo nafasi wako wengi wanaofaa sio Membe.
 
Aliyekuwa mgombea urais wa ACT Wazalendo kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 na akaishia kufanya kampeni kwenye kijiji cha Rondo huku akijinasibu kuwa anataingia na kufunga goli dakika ya 90 bwana Bernard Membe, leo mbele ya waziri mkuu ametangaza kumuunga mkono rais Samia na kusema yupo tayari kuwa kampeni meneja wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025!

Bwana Membe huwa anapenda kujitwisha sifa ambazo hana, ikumbukwe mwaka 2015 aliingia tano bora kwenye mchujo na kuishia kubwagwa hadi na kijana mdogo January Makamba.

Bwana Membe amekuwa waziri kwa miaka 15 lakini hakuna alichoifanyia nchi hii na wala hana legacy yoyote aliyowachia Watanzania

Membe asema yuko tayari kurudi mahali fulani | Mwananchi - Membe asema yuko tayari kurudi mahali fulani
Nyie tulieni dawa iwaingieni vzr, ndo tayar yupoyupo sana
 
Huyu Mzee mpaka leo simuelewi aliposema atasawazisha bao dakika ya 90!!?

Ni falsafa nzito sana mkuu. Ni kweli kama alivyo ahidi kachero mbobezi. Goli limefungwa. Sio dakika ya 90 bali dakika 90+7. Yaani sekunde za mwisho za dakika za nyongeza. Na sio tu kamshinda mpinzani wake bali “kamtupa nje kabisa ya mashindano yoyote yale na hatashiriki tena hadi kiama kitakapokuja!!!!!

Kachero mbobezi hakua nje ya uwanja. Alikua ndani ya mchezo hata kama watu walidhani ametolewa nje kwenda kugangwa majeraha.

Hakuwa punguani kutamka mbele ya kadamnasi kwamba atafunga goli dakika za majeruhi. Pale wadau wote walipo amini mchezo umekwisha na kachero kagaragazwa na wakawa wamemsahau na watu wakiamini timu aliyokua anapambana nayo imesonga mbele hata kama ni kwa mbeleko ya refa ndipo meza ilipopinduliwa kibabe!

Hakufunga goli yeye lakini alishiriki kimbinu kuhakikisha maneno na ahadi yake hayadondoki chini! Timu yake ilishinda na sote tulimuona akiibuka kutoka huko alipokua tukidhani anauguza majeraha na kuja hadharani kushangilia. Kumbuka huyu mtu hakutaka kabisa kusalimu amri tena katika kile kipindi ambacho ile timu kabambe ilikua na uwezo kwanza wa kumnunua mchezaji yoyote wanayemtaka na pili kuhakikisha yule asiyetaka hachezi tena maisha yake yote!!!

Amini nakwambia mkuu, goli la dakika za majeruhi ndio limefanya timu ile sasa hivi kua chali kabisa na timu kachero mbobezi inasonga mbele kwasababu wamethubutu na wameweza
 
Back
Top Bottom