Bernard Membe huna sifa wala uwezo wa kuwa 'campaign manager' wa Rais Samia

U
Mkuu naona unaanza kusahau mapema, ebu kumbuka enzi za hayati Dr John Pombe Magufuli akiwa waziri wa ujenzi!
Umenikumbusha mbali sana.
JPM akiwa Waziri wa Ujenzi alishikamana sana na TANROADS, kiasi kwamba alipopata Urais, Tanroads ukawa MHIMILI wa NNE wa Utawala.
Vyombo vya Habari, ambavyo katika Nchi zenye Demokrasia huwa Mhimili wa Nne, vikawatupwa pembeni kwa kunyanyaswa?
Rushwa ndani ya Tanroads, ambayo matokeo yake ni ujenzi wa Barabara zilizo CHINI YA VIWANGO, ilihalalishwa.
Hata CAG aliteuliwa kutoka Tanroads.
DG Bandari alitoka Tanroads.
DG Viwanja vya Ndege toka Tanroads.
Msimamizi Mkuu Bwawa la Nyerere toka Tanroads.
Mshauri Mkuu ujenzi SGR toka Tanroads!
Hakika, Tanroads iligeuka Mhimili wa NNE wa Taifa.
Na haikuwahi kukaguliwa na CAG.
Hakika, umenikumbusha mbali
 
Ninategemea wale vijana wa CCM wenye viherehere watamjibu Membe.
 
Bongo bwana, umaarufu alionao mtu mitandaoni nitofauti kabisa na uhalisia kwa wananchi wa kawaida(ambao kimsingi ndio wapiga kura)
 
Ujinga unaanzia kwenye kufikiria majina ya watu badala ya dira ya taifa na maendeleo ya watu! Natamani ifikie hatua mwenye maono makini ya kutuvusha apewe nchi aoingoze hata kama ni mgombea Binafsi!

Tumerudi nyuma sana! Tuamke!
 
Eti jasusi mbobevuuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].ukute ezekiel kamwaga akimsifuu sasaaa . utadhani ni bonge la jasusiii
 
Tokea Magufuli afe kuna watu wamekuwa wakiangaika kila kukicha nafikiri hawa ni wale waliokuwa wakinufaika na utawala ule wa kidhalimu na kikatili.
 
Nchi yetu inavituko sana, huyu ni kituko mwingine!!


Ila jamaa alitisha sana, eti kampeni hapigi halafu akasema ushindi ni asubhi tu na akasubiria dk za mwisho hahahhhhha wanasiasa wa bongoland /Africa vituko tupu
Eti ametenga 10b za kampeni[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na asithubutu hiyo nafasi wako wengi wanaofaa sio Membe.
 
Nyie tulieni dawa iwaingieni vzr, ndo tayar yupoyupo sana
 
Mimi nangojea kula hela za kampeni tu, masuala ya nani meneja hayanihusu😆
 
Huyu Mzee mpaka leo simuelewi aliposema atasawazisha bao dakika ya 90!!?
 
Huyu Mzee mpaka leo simuelewi aliposema atasawazisha bao dakika ya 90!!?

Ni falsafa nzito sana mkuu. Ni kweli kama alivyo ahidi kachero mbobezi. Goli limefungwa. Sio dakika ya 90 bali dakika 90+7. Yaani sekunde za mwisho za dakika za nyongeza. Na sio tu kamshinda mpinzani wake bali “kamtupa nje kabisa ya mashindano yoyote yale na hatashiriki tena hadi kiama kitakapokuja!!!!!

Kachero mbobezi hakua nje ya uwanja. Alikua ndani ya mchezo hata kama watu walidhani ametolewa nje kwenda kugangwa majeraha.

Hakuwa punguani kutamka mbele ya kadamnasi kwamba atafunga goli dakika za majeruhi. Pale wadau wote walipo amini mchezo umekwisha na kachero kagaragazwa na wakawa wamemsahau na watu wakiamini timu aliyokua anapambana nayo imesonga mbele hata kama ni kwa mbeleko ya refa ndipo meza ilipopinduliwa kibabe!

Hakufunga goli yeye lakini alishiriki kimbinu kuhakikisha maneno na ahadi yake hayadondoki chini! Timu yake ilishinda na sote tulimuona akiibuka kutoka huko alipokua tukidhani anauguza majeraha na kuja hadharani kushangilia. Kumbuka huyu mtu hakutaka kabisa kusalimu amri tena katika kile kipindi ambacho ile timu kabambe ilikua na uwezo kwanza wa kumnunua mchezaji yoyote wanayemtaka na pili kuhakikisha yule asiyetaka hachezi tena maisha yake yote!!!

Amini nakwambia mkuu, goli la dakika za majeruhi ndio limefanya timu ile sasa hivi kua chali kabisa na timu kachero mbobezi inasonga mbele kwasababu wamethubutu na wameweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…