Bernard Membe, kama basi limekuacha chukua pikipiki ufike

Kwenye Jamii kuna Makundi mawili la watawala na watawaliwa, watawala hawawezi ruhusu katiba inayowabana
 
Mikwara ehe! Ngoja utashangaa mpaka uzimie. Unajua watu wa CCM walio naye bega kwa bega? Ni watu wazito na hata kama watahamia chama chovu kama TLP Magufuli + dola hawataweza kuzuia huo mshindo.
Ukishakuwa nje ya mfumo na wanufaika awapo upande wako huna chako ukakune nazi tu
 
Kachero Mbobezi Bernard Kamilius Membe
 
Hiki ulichoandika hapa ndicho nilichokiandika pale mkuu.
Kwenye Jamii kuna Makundi mawili la watawala na watawaliwa, watawala hawawezi ruhusu katiba inayowabana
 
Waliokuwa kwenye system then wakashindwa kuibadilisha systems ili iwafae hata siku systems ikiwatupa wapambane na Hali yao
Watu wanapojisahau kuwa mfumo wa hovyo waouendekeza na wanaojidanganya kuwa wao hautawadhuru kana kwamba mhanga si Mtz mwenzao, sasa yanawakuta, nae anadai tume ya uchaguzi!
 
Kachero kachanganyikiwa kawa kama samaki nje ya maji hana ujanja,anangángánia CCM utadhani CCM ni baba /mama yake aende kwa akina Mbowe au Zitto ndio apambane na JPM,CCM wamemtupia virago baado tu anangángánia kama si kukosa busara ni nini sasa.
 
Na kama anajiona anakubalika na WaTz, basi angeanzisha chama chake akapata wafuasi lukuki watakaomuunga mkono.

Asing'ang'anie Ccm walikomfukuza!

Kung'ang'ania ng'ang'ania huku mwishowe ataonekana amechanganyikiwa na kwamba sindano ya kufurushwa imemwingia barabara!
 
Ajitahidi kuwa mwangalifu asijepata ajali maana pikipiki ni risk Sana na inahitaji uzoefu hasa Kama unafukuzana na mabasi ya kisasa yana Kasi Sana pia mashimo ya barabara za lami ni hatari.
 
Leo ndio anakumbuka kwamba inatakiwa iwepo tume huru ya uchaguzi. Walipokuwa ndani ya mfumo walichekelea leo wametolewa wanalilia.

Simpendi Jiwe ila sometimes ni afadhali anavyowanyoosha hadi nzi wa kijani wenzie. Ili hata wanaotamba sasa hivi wajue ipo siku mfumo utawabwaga, hivyo watumie muda huu kutengeneza katiba bora ikiwemo tume huru ya uchaguzi.

Acha akome.
 
Mkuu kuachwa au kuachika kwa gafla kubaya na kunaumiza sana, pamoja na siasa kitakiwa kucheza kwa akili wengi wakiwa na nguvu humo humo ndani wanajisahau kuwa hiyo nguvu imeegemea nini..!.

Mfano hapo jamaa anasema ana watu wazito kama 6 na yeye wa saba, hata hao 6 najua kwa sasa kila mmoja anajitafakari endapo watachukua uhamuzi mgumu what next baada ya uhamuzi wao.

Kweli kama unataka mabadiriko using'ang'ani pale ulipo toka ili uonyeshe tofauti yako na aliye ndani lakini wengi hata wakitoka wanashindwa hii ni kutokana na mfumo uliopo unampa nguvu kubwa akiyeshika mpini, ukija kwa wananchi ndiyo kabisaaa, hofu na mashaka juu yako inakuwa kubwa ukiwa nje.
 
Membe anatumika na ccm kuwafanya vichwa panzi wasahau kuhusu upinzani. Mkija kushtuka Mbowe ameuza chama kwa Membe kama alivyokiuza kwa Lowasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…