Bernard Membe: Kuna umuhimu wa kufanya vetting kwa viongozi wetu kuhusu uraia na afya zao

Maembe anazidi kuonesha alivyo zero brain.
Anajiita afisa wa TISS na mtu ya sisistimu (system) alishindwaje kuleta jalada la uraia wa watu wasiokuwa raia na leo wamekuwa viongozi!?

Ama si yeye Bali ni maembe mwingine anayehojiwa na hili gazeti!?
 
Kama sio dr .magufuli hata ccm ya 2015 ilikuww hoi bin taabani kila aina ya takataka ilikithiri awamu 4 .awamu ya 5 ndo iliyoipa heshim sisim kila kijana akawa anajivunia kuingia ccm sio upinzani hata ccm wenyewe
 
Ina maana Jiwe alikuwa anawasha mziki na kucheza peke yake?
 
Hata mchonganishe vipi Magufuli ni msukuma tena kwa wazazi wake wote na majina yao ni kisukuma,mnajaribu kuwachonganisha wasukuma fala nyie hamtaweza

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
“Tusipofanya vetting ya viongozi kiafya tunaweza kuwa na watu wa magonjwa ya akili. Sikufichi, katika kipindi hiki nilipoona kiongozi aliyepewa dhamana yuko ofisini kwake anawasha muziki anacheza peke yake na kujirekodi, halafu mnamuangalia mtajua kuna tatizo. Ukiona kiongozi amefikia hatua hiyo, ujue kuna tatizo na hatujafanya vetting vizuri,” anasema Membe.
Kwanini alijiunga ACT-Wazalendo?
[emoji23][emoji23][emoji23] Uzee shida sana, wazee wanacheza ofisini
 
kwani katiba inasemaje kuhusu uraia? huyu bm naona kama anachanganyikiwa. Vp anaiongelea sana ccm na si ACT alipotoka
 
Nimejaribu kuisoma hiyo habari hapo juu,nimeona ni uchafu na takataka.Hivi Marehemu Raid wetu Magufuli baba yetu,hawa watu wa hovyo hovyo watamweza kweli?Ahaaa wapi!!Hata wakiungana !!Kwa ufupi hata hill gazeti pia ni uchafu na taka taka.Eti Magufuli ni Mrundi?Ndio maana nyerere alikuwa hapendi ujinga na uchafu wa ukabila.Yaani Member ana matope tupu kichwani.Hivi alifikaje kuwa waziri?Ukianza kudai makabila ya watu hakuna atakaye baki.Nyerere mwenyewe alitoka Rwanda.Member mwenyewe ni Mmakonde wa Msumbiji.Mm mwenyewe ni mruri wa Musoma.Lakini unaambiwa tumetoka Cameroon. Kwa ufupi kilichoelezewa na Member na kuandikwa na kigazeti cha kufungia maandazi ni uchafu na matope tupu.Magufuli ,yule ni chuma sio MTU wa kawaida kama wasaka uteuzi na watokao mafichoni.
 
Kwahiyo Kikwete alimpa Uwaziri bila vetting? Nini kazi ya idara ya usalama wa taifa, ambapo hutuaminisha ni mmoja wao tena akiwa mbobezi, kama walishindwa kulisaidia taifa kung'amua kitu ambacho ni common sense, shame on them!!!
 
Kwa makala hii iliyobandikwa kupitia mwandishi wa habari wa Jamhuri hapana shaka mhusika wa kifo cha JPM amejulikana bayana na kumbukumbu imewekwa wazi kwa wasiojua kuvunja kifungo cha siri (confidential details code patterns breaking and decoding).

1. Membe anachuki binafsi dhidi ya hayati JPM, Dr Bashiru Ally na Humphrey Polepole
2. Alicheka alipoombwa kurejea CCM baadae Mungu akaingilia kati
3. Aliwachukia hayati JPM na Maalim Seif Sharif Hamad ndio maana alikataa kwenda kuwazika na bado hajutii umamuzi huo!!!!
4. CCM ni uchawi
5. Kuna viongozi ngazi za juu srikalini na CCM sio raia wa Tanzania na ukweli aliujua akiwa upinzani halafu anajiita kachero mbobezi!!!
6. Anadai serikali ya awamu ya nne pekee ndio pekee ilikuwa inafanya 'vetting' makini kubaini viongozi wanaofaa wakati akijua awamu hiyo hiyo kulikuwa na mamluki wapo ikulu!!!
7. Aliungwa mkono na watu wa Lindi na Mtwara halafu anjipa matumaini angeweza kuongoza nchi ya Tanzania kwa kura za watu wasiomtaka
8. Kwa kuwa kuna mtu tayari amejitokeza hadharani kupitia chombo cha habari kudai aliwachukia hayati JPM na Maalimu Seif basi viongozi hao hawakufa kwa ugonjwa wa utashi wa mwenyezi Mungu mhusika amejifunua yeye mwenyewe bila shinikizo kutoka kwa mtu yeyote

Pole sana Tanzania mtaendela kutoa machozi na hamtaweza kuwa na viongozi waliojitoa wakadumu kamwe kwa kuwa hata ninyi hamjali kuhoji na kuchukua hatua dhidi ya viongozi wenye uchu wa madaraka kutumia njia ovu kuwaumiza.
 
Awamu ya nne ingekua makini katika Vetting Magufuli na Dk. Mpango wasingefika walipofika...

Afterall Tanzania ni kama marekani tu ni ardhi ya wahamiaji.
Uraia wa Dr. Mpango nao una mashaka mkuu? Drop some more details pls.
 
The Returns of the Champions
Waswahili wanasema mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.

Jasusi hili CCM ndipo ngamani pake huko Act Wazalendo ni tezini na harakati zake za kimaisha ni omoni pake ila ngamani pale ni CCM.

Wenye nyumba wameamua kurudi mazima,kama mbwai na iwe mbwai yaani ukijua ya mbele sisi tunajua ya nyuma enewei wacha Kazi Iendelee..
 
Kumbuka amekuwa ndani ya chama kwa miaka zaidi ya 40 na kushika nafasi nzito ndani ya mfumo. Pili hatuwajui hao wazee na wajumbe wa CC waliokuwa wakimpigia simu kumshawishi arudi chamani so mpaka kuongea hivyo maanake ameshajiridhisha kuwa maneno yake hayatasababisha madhara au mpasuko wowote kwa walimpo ndani ya chama na mfumoni.
 
Mzee bado anakifukuto..........

Kipande cha maumivu na huzuni bado kitaendelea kuwepo kwa sababu ya tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…