beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Kachero ni kachero tu!
Najua sitavunja sheria wala kanuni hapa.
Bernard Membe, Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya ACT Wazalendo 2020. Historia yake ya kisiasa na utumishi inajulikana. Itoshe tu kusema ni Mtanzania ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kisiasa na kitaifa.
Tangu sekeseke lake na CCM/Magufuli litokee na kumfukuzisha uanachama, swali moja la msingi sana nimekuwa nikijiuliza ambalo pengine kupitia humu tunaweza kusaidiana kupata majibu.
Labda niulize; kwanini Membe hamtaji kabisa Rais Magufuli kwa jina lake katika kauli zake anazozitoa? Mara zote amekuwa akimtaja kama fulani, bwana yule au kumrefer kivingine bila kumtaja directly. Ni kama anakwepa kumtaja jina hata akiwa anatoa speech kinzani. Je, ni kwa sababu ana kiapo cha utii cha ukachero? Kiapo kinachomzuia kumkosea heshima boss wake?
Ikumbukwe, kanali Lubinga aliwahi kumuonya na kumtahadharisha Membe >> Kanali Lubinga: Membe anaweza kushtakiwa kwa kumshambulia Amiri Jeshi Mkuu. Akumbuke kuna Court Martial, aheshimu kiapo
Kama ndivyo, uwepo wake nje ya system una maana gani kama bado anatakiwa kutii kiapo?