Mkuu The Boss, nakupa kongole kwa hoja murua ambazo umezianisha. Lkn nafikiri ni lazima tuangalie mazingira ambayo matukio ya mabadiliko yanapotokea, hali kadhalika na usimamizi wake unavyokuwa.
Kipindi cha Mrema alikuwapo Mwl. Nyerere, ambaye aliweza kuzuia mabadiliko kwa hoja murua kabisa, na hata kuweza kumnadi barabara mgombea wa CCM aliyeteuliwa. Baada ya Mkapa lilikuja kundi la mtandao ambalo liliweza kufanikisha chaguo lao na hata kuweza kumpa JK hatamu za uongozi wa awamu ya nne.
Awamu ya tano imekuja kwa uongozi wa bahati nasibu. Hali ambayo ilitokana na wanamtandao kukosa mrithi wa JK na hatimaye kujikuta wote wakiikosa nafasi ya mmoja wao kumrithi mtu wao.
Ujio wa JPM ulikuwa kama embe dodo ambalo limeokotwa pasipo kutarajia. Hali ambayo imempelekea kuendesha siasa kwa hisia badala ya msingi ya chama. Sasa kinachokea kwake ni kuwa ametengeneza uadui na CCM Asilia na kuamua kuambatana na machotara wa siasa andamizi.
Mkuu, kwa vyovyote vile, tusijaribu kulinganisha jitihada na matokeo ya vita hivi vya kugombea madaraka kwa mazingira ya sasa ya kisiasa. Membe bado ni mtu muhimu ambaye anaweza kubalisha "rules of the game" za siasa za wakati huu hapa nchini.