Bernard Morrison (Ben Maokoto) awajaza kwenye rada Waarabu

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Mchezaji wa Kimataifa wa Ghana mtukutu Benard Morrison au BM3 au Ben Maokoto au vyovyote vile utakavyomwita awajaza Waarabu kwenye Rada yake. Na hatimaye wamejaa.

Pamoja na kutokuwa na imani naye kutokana na faili lake kutokuwa zuri kwenye Timu zote alizopita kwa shingo upande AS FAR RABAT wamemkabidhi mkataba wa mwaka mmoja ambao unamfanya BM3 kuwatumikia mpaka mwaka 2024.

Baada ya kuona hawana mpango naye Mtukutu aliamua kuwaonesha uwezo wake uwanjani baada ya kubaini mapungufu ndani ya kikosi naye akapitia humo humo.

Huyu ndiyo BEN MAOKOTO akiamua anaweza.
 
Ben ni mchezaji huru na ukiacha shida ya kinidhamu mpira anaujua, vilevile kwenye fursa anajiongeza na vitu uwa rahisi ukiweza kujiongeza ndivyo dunia ya soka inavyo kwenda.

Usione Boko haondoki Simba ukafikiri ni ndumba pekeyake anajua kuishi na viongozi wake vizuri kwakua mkono mtupu haulambwi.
Usione kule Ulaya Philip Jones anaumwa kila siku lakini mkataba hauvunjwi na analipwa mshahara kufulu ukadhani yanatokea kwa bahati mbaya.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Morrison anaujua vizuri mpira, shida yake ilikuwa nidhamu tu. Yanga haikupaswa kumwacha huyu jamaa afu unabakia na akina Mzize.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Utakaaje na mchezaji kama Morrison?

Unajuwa Morrison anacheza namba ngapi na hiyo nafasi yake kuna wachezaji gani?

Mzinze ni product ya Yanga kama alivyokuwa Mkude Simba, huwezi kumuacha ili ufurahishwe mtu kama wewe usiyejuwa Yanga wamewekeza kiasi gani kwake.

Mzinze bado hajaiva lakini bado anao muda wa kuleta furaha Jangwani akiongeza bidii.
 
Kuna projects ambazo ni failure, Mzize ni very average player, usitarajie kuna siku atakuwa tegemeo kama akina Mayele. Hapo alipo ndio kaiva.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…