Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Dkt. Kizza Besigye, mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda anayeshikiliwa rumande, amefungua shauri mahakamani dhidi ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, akidai kuwa amekuwa akitoa matamshi ya hadharani yanayotishia maisha yake na hivyo kuhatarisha haki yake ya kupata usikilizwaji wa haki katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Katika maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu ya Kampala, Besigye anadai kuwa Jenerali Muhoozi, ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, amekuwa akitumia mtandao wa X kutoa kauli mbalimbali dhidi yake tangu alipokamatwa Nairobi, Kenya, mwezi Novemba 2024.
Mbali na vitisho hivyo, Besigye anapinga pia kauli zinazomtaja kama mhalifu kabla ya mahakama kutoa uamuzi, akisema matamshi hayo yanakiuka haki zake za msingi na yanaweza kuathiri mwenendo wa kesi.
Vilevile, anaiomba mahakama itangaze kuwa mashtaka ya uhaini na kuficha taarifa za uhaini yanayomkabili hayazingatii misingi ya haki za binadamu, utawala wa sheria na haki ya kusikilizwa kwa haki, hivyo hayapaswi kuendelea.
Katika kesi hiyo, Besigye ametaja pia maafisa wa jeshi la Uganda, Kanali Peter Ahibisibwe na Luteni Kanali Ephraim Byaruhanga, akiwatuhumu kuhusika katika madai ya kutekwa kwake Nairobi kabla ya kupelekwa Uganda.