Best Hip-Hop MC's of all time Bongo (Top five)

Geez Mabovu na Roho saba hawamo?
Geez pia ni mkali sana ila binafsisioni akiwa na ngoma nyingi. Kwa mfano hapo juu nimemuweka mtu kama Balozi Dolla Soul ingawa pia hakua na ngoma nyingi.
 
Na Chidbenz kuwa juu ya Nikki mbishi jaribu kufanya tathmini tena may be umefanya conclusion ukiwa umebase kwenye upendo ila tukiangalia facts Chidbenz adeserve kuwa juu ya Nikki mbishi.
Nikki mbishi ni over rated mc wa watu wanaoamini kwenye hip hop asili

To be honest napenda sana muziki lakini siujui wimbo hata mmoja wa Nikki mbishi kama ninavyo zijua za Chid benz

Hawa wako ulimwengu tofauti kabisa mkuu, enzi za Chid Benz alikua anajaza show, man alone. huyo Nikki hata ukiweka bure baa nani atakwenda? Labda abebwe kwenye matamasha

Nikki atabaki msanii wa mtaani tu àmbaye kipaji chake haki msaidii ku make money and fame..... hili ndio lengo

Hata USA kuna jamaa mitaani wanachana balaa hadi wakina Nass jay z nk wanasubiri
Lakini hawawezi kutajwa ma Mc wakali kuliko akina Jay z
 
Usitake kila mc avume ndo afikie vigezo unavyovitaka.
Dunia ipo hivyo sio kila mtu atafanana na mwenzie ndomna kuna mainstream mcs na underdowgs kila sehem ipo hivyo.
So wakati wewe ukisema mbishi sijui hatojaza ukumbi wakati kuna raia hawakosi kumsupport kwa kazi zake.mwisho wa siku kila mtu abaki na kusikiliza na kusupport anachopenda na sio kutaka mc afanane na wengine kwa ajili ya fame nk
 
Wenyewe mnaita ma Mc wanaofuata nguzo tano za Hip Hop......
 
1.Profesa Jay
2.Fid Q
3.Binamu
4.Ngwea
5.Jay Mo
 
Yaani utaje Hip Hop ya bongo usimtaje Sugu kama The God Father...?

Sugu ana album 11 hakuna yeyote hapo juu mwenye idadi hii ya Albums.

Hits kama Ni Wapi Tutakwenda...Mambo ya Fedha ...Chini ya miaka 18...Niko Makini...Mikononi mwa Polisi....Sugu...Mambo ya Fedha...Moto Chini na Deiwaka nk. huku nyingi tu zikienda bila ya Promo za Clouds au Radio fulani bali watu walinunua Album zake kwa kuamini uwezo wake.

Kulikua na wababe kama Kwanza Unit...Hard Brasters....GWM...Diplomats..yaani kifupi Mcs kama kina Zavara...Saigon..Ramson..Balozi...Fanani nk lakini bado Sugu akatoboa na kua no 1 yaani siyo kwamba mambo yalikua simple.
Ushamsikia Sugu kweye Collabo ya Hit song ya muda wote Kama ya Yamenikuta ya GWM?ambayo hadi leo ni slogan mtaani,watu husema "Yamenikuta Mzee Mwenzangu"

Sugu amevitoa vichwa kama Mfalme wa Rhymes Afande Sele na Malkia wa Muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee....nikimaanisha hawa wote kwa mara ya kwanza wamesikika kwenye nyimbo za mkongwe huyu Sugu.

Sugu ndo mwanzilishi wa Tanzania Hip Hop Summit achilia mbali Antivirus mambo yalipokua magumu kwa baadhi ya wasanii.

Master Jay amewahi kukili kuwa Album ya Sugu ya pili ambayo ni Ndani ya bongo ndiyo ilimfanya awe producer seriously.

Huyu ndo Mentor wa Prof Jay kwenye siasa na baada ya mwana HipHop..Mwana harakati Sugu kuwa mbunge kila msanii anaoona inawezekana..WHY? Because yeye ni GOD FATHER wao.Rejea pia kesi ya Afande Sele,Baba Levo NK.

Kwa research yangu ndogo bwana Joseph Mbilinyi..au Mr 2..au 2proud Rais wa Mbeya Sugu ndiye God Father siyo tu wa Hip Hop ya Bongo bali Muziki wa Kizazi kipya yaani bongo Flava kwani ameshawahi kupafom akiwa peke yake kama msanii wa Bongo Flava pekee huku wengine wkiwa ni wasanii wa muziki wa Dansi kwenye Tamasha la Mazingira lililoandaliwa na Mzee John Kitime mwaka 96 na kufunika vibaya na Songi lake la ni WAPI TUTAKWENDA kitu alichokirudia mwaka jana ndani ya Bunge la Tanzania alipopafom Songi lake la Chini ya 18 na kumuacha muheshimiwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wengine wakitikisa vichwa wakati mistari konde ikipenya medula zao.
Tuishie hapo tu ila kuna mengi kuhusu huyu God Father Sugu Hujamtendea haki hapo juu mkuu...fanya utafiti vizuri ili uje umtangaze upya the Real God Father..or else tutazidi kupaza sauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…