Best Hip-Hop MC's of all time Bongo (Top five)

Best Hip-Hop MC's of all time Bongo (Top five)

Na Chidbenz kuwa juu ya Nikki mbishi jaribu kufanya tathmini tena may be umefanya conclusion ukiwa umebase kwenye upendo ila tukiangalia facts Chidbenz adeserve kuwa juu ya Nikki mbishi.
Nikki mbishi ni over rated mc wa watu wanaoamini kwenye hip hop asili

To be honest napenda sana muziki lakini siujui wimbo hata mmoja wa Nikki mbishi kama ninavyo zijua za Chid benz

Hawa wako ulimwengu tofauti kabisa mkuu, enzi za Chid Benz alikua anajaza show, man alone. huyo Nikki hata ukiweka bure baa nani atakwenda? Labda abebwe kwenye matamasha

Nikki atabaki msanii wa mtaani tu àmbaye kipaji chake haki msaidii ku make money and fame..... hili ndio lengo

Hata USA kuna jamaa mitaani wanachana balaa hadi wakina Nass jay z nk wanasubiri
Lakini hawawezi kutajwa ma Mc wakali kuliko akina Jay z
 
Nikki mbishi ni over rated mc wa watu wanaoamini kwenye hip hop asili

To be honest napenda sana muziki lakini siujui wimbo hata mmoja wa Nikki mbishi kama ninavyo zijua za Chid benz

Hawa wako ulimwengu tofauti kabisa mkuu, enzi za Chid Benz alikua anajaza show, man alone. huyo Nikki hata ukiweka bure baa nani atakwenda? Labda abebwe kwenye matamasha

Nikki atabaki msanii wa mtaani tu àmbaye kipaji chake haki msaidii ku make money and fame..... hili ndio lengo

Hata USA kuna jamaa mitaani wanachana balaa hadi wakina Nass jay z nk wanasubiri
Lakini hawawezi kutajwa ma Mc wakali kuliko akina Jay z
Usitake kila mc avume ndo afikie vigezo unavyovitaka.
Dunia ipo hivyo sio kila mtu atafanana na mwenzie ndomna kuna mainstream mcs na underdowgs kila sehem ipo hivyo.
So wakati wewe ukisema mbishi sijui hatojaza ukumbi wakati kuna raia hawakosi kumsupport kwa kazi zake.mwisho wa siku kila mtu abaki na kusikiliza na kusupport anachopenda na sio kutaka mc afanane na wengine kwa ajili ya fame nk
 
Usitake kila mc avume ndo afikie vigezo unavyovitaka.
Dunia ipo hivyo sio kila mtu atafanana na mwenzie ndomna kuna mainstream mcs na underdowgs kila sehem ipo hivyo.
So wakati wewe ukisema mbishi sijui hatojaza ukumbi wakati kuna raia hawakosi kumsupport kwa kazi zake.mwisho wa siku kila mtu abaki na kusikiliza na kusupport anachopenda na sio kutaka mc afanane na wengine kwa ajili ya fame nk
Wenyewe mnaita ma Mc wanaofuata nguzo tano za Hip Hop......
 
1.Profesa Jay
2.Fid Q
3.Binamu
4.Ngwea
5.Jay Mo
 
G.morning everyone,
Me ni big fan wa hip-hop ya bongo, na katika research nlioifanya hii ndo list yangu ya MA mc bora wa muda wote waliowahi kutokea hapa Tanzania

1) Professor j,
Huyu jamaa anabaki kuwa no 1 kwa muda wote kutokana na uwezo wake binafsi wa Utunzi wa mashairi na uwezo wa kuandika na kusimamia kwenye Mada anayoielezea tofauti na MA mc wengine Ambao Unakuta jina LA nyimbo na maudhui ya nyimbo yanalandana, pia n mc pekee mwenye nyimbo nyingi Kali zilizogusa mashabiki wa kila Aina na ni moja ya inspirations kwa new upcoming hip-hop artists
Naweza kumuita God father wa bongo, ktk industry ya music.

2) Albert mangwea & j. Moe
Hawa jamaa kwangu wanashika no 2 kwa pa1 coz wana uwezo ambao almost unalingana, ukiangalia nyimbo km kimya kimya, kimafia. N
K waliofanya colabo Wote utagundua uwezo wao n km unafanana, achilia mbal uwezo wa ngwair kwenye free Style.. Na Utunzi wa j.moe akiwa anaelezea story. Wanabaki kuwa best rappers wa muda wote.

3) Chidibenz
Huyu mfalme wa Ilala ni mc hatari Sana,ana vocal na michano mikali sana na pia ana uwezo Mkubwa sana kwenye performance, wengi mnakumbuka enzi zake kwenye kila collabo alikua anakimbiza, Huyu km angepata manager mzur, na angepunguza kiburi jamaa Angekua Mbal sana, kwa Mimi nampa no 3 kwa ubora wake.

4) Langa & Fid q
Hawa jamaa kwa pa1 nawapa nafasi ya nne, Fid q anauwezo Mkubwa wa kuandika vitu ambavyo viko deep sana na km n mtu unayesikiliza juu juu pengine unaweza usione Au usielewe kabisa ubora wake, Langa alikua na uwezo Mkubwa sana wa ku spit kingereza na kiswahili Hakua na mistari konde Ila alikua anaandika vitu deep sana, kwa mtazamo wangu Langa na fid q wanauwezo unaofanana tofauti n kuwa Langa mpaka anatutoka Hakuwa na project nyingi lakini ukisikiliza nyimbo zake utatambua uwezo wake, my favorite line ya Huyu jamaa ni (hawanichekei usoni kisogoni wananisema wanatafuta mabaya wanajifanya Hawaoni mema).

5) Nikki mbishi (Baba Malcom)
Huyu jamaa ni mkali sana kwenye uandishi na flow anauwezo Mkubwa wa ku free style, ana punch za maana na ngoma ambazo n classic, changamoto nnayoiona kwa Huyu jamaa ni ana km kiburi flan Hv ana attitudes za ajabu ajabu km kudis wanasanii wenzake na ujuaji mwingi.. Ila ni mc hatar sana
Apart from hao top five pia wapo Mc's wengine wakali km stereo, one the incredible, Godzilla, p the mc country boy, na wengine wanaofanya vizuri

Kindly regards
Dagger-v
Yaani utaje Hip Hop ya bongo usimtaje Sugu kama The God Father...?

Sugu ana album 11 hakuna yeyote hapo juu mwenye idadi hii ya Albums.

Hits kama Ni Wapi Tutakwenda...Mambo ya Fedha ...Chini ya miaka 18...Niko Makini...Mikononi mwa Polisi....Sugu...Mambo ya Fedha...Moto Chini na Deiwaka nk. huku nyingi tu zikienda bila ya Promo za Clouds au Radio fulani bali watu walinunua Album zake kwa kuamini uwezo wake.

Kulikua na wababe kama Kwanza Unit...Hard Brasters....GWM...Diplomats..yaani kifupi Mcs kama kina Zavara...Saigon..Ramson..Balozi...Fanani nk lakini bado Sugu akatoboa na kua no 1 yaani siyo kwamba mambo yalikua simple.
Ushamsikia Sugu kweye Collabo ya Hit song ya muda wote Kama ya Yamenikuta ya GWM?ambayo hadi leo ni slogan mtaani,watu husema "Yamenikuta Mzee Mwenzangu"

Sugu amevitoa vichwa kama Mfalme wa Rhymes Afande Sele na Malkia wa Muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee....nikimaanisha hawa wote kwa mara ya kwanza wamesikika kwenye nyimbo za mkongwe huyu Sugu.

Sugu ndo mwanzilishi wa Tanzania Hip Hop Summit achilia mbali Antivirus mambo yalipokua magumu kwa baadhi ya wasanii.

Master Jay amewahi kukili kuwa Album ya Sugu ya pili ambayo ni Ndani ya bongo ndiyo ilimfanya awe producer seriously.

Huyu ndo Mentor wa Prof Jay kwenye siasa na baada ya mwana HipHop..Mwana harakati Sugu kuwa mbunge kila msanii anaoona inawezekana..WHY? Because yeye ni GOD FATHER wao.Rejea pia kesi ya Afande Sele,Baba Levo NK.

Kwa research yangu ndogo bwana Joseph Mbilinyi..au Mr 2..au 2proud Rais wa Mbeya Sugu ndiye God Father siyo tu wa Hip Hop ya Bongo bali Muziki wa Kizazi kipya yaani bongo Flava kwani ameshawahi kupafom akiwa peke yake kama msanii wa Bongo Flava pekee huku wengine wkiwa ni wasanii wa muziki wa Dansi kwenye Tamasha la Mazingira lililoandaliwa na Mzee John Kitime mwaka 96 na kufunika vibaya na Songi lake la ni WAPI TUTAKWENDA kitu alichokirudia mwaka jana ndani ya Bunge la Tanzania alipopafom Songi lake la Chini ya 18 na kumuacha muheshimiwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wengine wakitikisa vichwa wakati mistari konde ikipenya medula zao.
Tuishie hapo tu ila kuna mengi kuhusu huyu God Father Sugu Hujamtendea haki hapo juu mkuu...fanya utafiti vizuri ili uje umtangaze upya the Real God Father..or else tutazidi kupaza sauti
 
Back
Top Bottom