I hope umejibu kulinganisha na kile mleta maada alichodai hapa (best roads in Africa) na nilichomjibu kwa kuweka statistics (ambazo zinahusisha financier wa roads infrastructure hapa nchini). Sijahusisha paved kilometres as a row data (kama ulivyofanya wewe). Nitakupa mfano: Mauritius wana chini ya 2000km zenye lami lakini ni 98% paved, Morocco wana 70.4%, Botswana 37% etc. Sasa tukianza kujisifia kuwa tuna best roads network in Africa, tunajilinganisha na Africa ipi?
Nimekujibu kulingana na data ulizozileta mwenyewe kwamba only 6 578km or 7% of the total road network is paved.
Ndio nikakupa mifano ya baadhi ya barabara ambazo ziko PAVED yaani zenye lami.
Sasa nijibu...wewe unaamini kuwa network ya barabara Tanzania zenye lami (paved) ni hizo 6,578 km au 8,000 km? Hii si unaweza fanya homework mwenyewe na kujua makadilio ya km zenye lami TZ? Serious useme only 8K km ni paved in TZ? Duu...basi kazi ipo...kama hatujikubali wenyewe...ni tatizo kwa jamii yetu.
Kuhusu ubora, ukilinganisha EA...naamini Network ya barabara nyingi Tanzania ni bora kuliko hao majirani zetu (Not Africa yote maana sijatembelea nchi zote za Africa) lakini kwa EA hasa KE, UG hawawezi fikia ubora wa barabara za Tanzania...hili hata wewe mwenyewe you'll note the difference ukidrive kwenye hizo nchi. Na kizuri TZ barabara zimesambaa kote kote yaani sio tu Dar...
Nadhani hii pia inachangiwa na upya wa barabara nyingi Tanzania na controlled weight ya magari makubwa ndo inafanya barabara hizi ziwe bora..... mkuu unaweza safiri na Vitz from North of TZ to South, East to West bila shida yeyote na hata kuona shimo barabarani....je tusiite barabara bora?