Best Tanzanian radio and TV ads

Best Tanzanian radio and TV ads

Yule mzee fataki kwenye tangazo la "SIDANGANYIKI" napoambiwa sidanganyiki
huwa kuna pozi moja analiweka akimcheck kifataki fataki binti...huwa ananiacha hoi sana
hahahahhaha
 
Lile tangazo la haki kwa watoto wa kike wajawazito kusoma..hehehe

jamaa anaongoza kikao anasema eeh jamani kama mnavyoona mi napenda sana
watoto hawa waendelee na shule lakini wezangu hawatakiii kabisa...

Binti mjamzito anatokea, zee linanong'ona yule mwanafuzi mjamzito anafanya nini
hapa..huu si ndo umalaya mwambie aondoke haraka ..hahahahahahaha
 
Mie naona matangazo yote ya Tigo- mwaka huu yalikuwa bomba sana.
 
na midude ile ya fataki ni mizuri na imejaa ubunifu wa hali ya juu ile mbaya.
Kweli mjomba mpoto ni msanii aliyeiva

Sure.
Tangazo la fataki linaloniacha hoi ni lile ambalo ameigiza na Natasha (Susan Lewis) ambalo fataki anataka kumhonga simu na gari mtoto wa Natasha, na Natasha anawafuma na kusema 'Mguu huu ni moja kwa moja hadi kwa mkeo, mja wa laana wewe'!
Mshituko alioupata Fataki sipati picha katika real world unakuwaje?
 
..Mi kwa kweli nilivutiwa sana na tangazo la serengeti kabla hawajali-edit. Kulikuwa na demu mmoja amevaa gauni white anakatika kiuno mbaya. Sijui kwa nini walimtoa yule nilikuwa na mpango wa kumtafuta Teddy Mapunda PRO wa Serengeti anipe details zaidi...Lakini mpango bado pale uko pale kile kiuno anachokata yule manzi kinanikumbusha mbali sana!!!
 
..... Kulikuwa na demu mmoja amevaa gauni white anakatika kiuno mbaya. ...


Teh teh teh!
Ulipoanza na ....."Kabla hawaja-edit"... nikajua moja kwa moja kwamba kuna kitu umekikosa! Yule mwanadada alibamba attention za tulio wengi, alikuwa ananengua ile mbaya!
Watu mna kumbukumbu, duh!
 
Uhuru wa kuongea (zain), fataki, na yote ya tigo.
 
Hivi kuna ambao mmewahi kuona tangazo la dstv???
Ambalo mtoto anamuimbia baba yake happy birthday
halafu baba anaanza kumkosoa mtoto
sauti haina punch,kipaji hakuna???
Tangazo zuri sana.
 
lililo niacha taabani nilile tangazo tigo la yule jamaa alipotumiwa sms ya kumtukia salio mwenzake akaanza kukumbuka mema aliyofanyiwa na mwenzake teh teh
 
lililo niacha taabani nilile tangazo tigo la yule jamaa alipotumiwa sms ya kumtumia salio mwenzake akaanza kukumbuka mema aliyofanyiwa na mwenzake teh teh
 
Back
Top Bottom