Hapa bado kuna kitu sijaelewa. Kama Mtoto anaanza Darasa la 1 akiwa na Umri wa Miaka 6, atahitimu Darasa la 7 akiwa na Miaka 12 na hivyo kuwa Kidato cha 4 akiwa na Miaka 16! Hivyo kama uzi huu ni uthibitisho wa kuwepo hapa kwenye Mtandao wa Jamii Wanafunzi wa Sekondari kama Members basi kuna watoto wa Shule Members wenye miaka 17, 16 na pengine chini ya hapo. Hiyo ni hatari kubwa! Wazazi wa Kizazi cha .com tuka kazi kweeelikweli!