Bethel Secondary School

Ng'wale

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Posts
4,690
Reaction score
3,399
Kwa wale wanaoifahamu hii shule nasikia iko Mafinga. Ningependa kupata maelezo yake kuhusu ubora wa taaluma, mahali/sehemu ilipo kwa huko Mafinga na kama ni mchanganyiko na mengine mengi. Natanguliza shukrani mbele.
 
Ni ya wasichana tu ila nasikia inafanya vizuri sana nakushauri peleka mwanao pale
 
Ipo mafinga maeneo gani?
 
Google kwanza matokeo yake necta kwa form four zilizopita ndipo utaupata ukweli zaidi. Mimi shule nzuri ni ile inayocheza nafasi yoyote katika kumi bora follows twenty bora, thirty bora kitaifa. Kwenye necta wameweka band ya kijani high petforming schools na ni top ten zote, followed by yellow ambazo ni medium performing schools and red low performing schools ambapo shule nyingi zimetumbukia humu. Kwa wale mnaotegemea kuanza mchakamchaka wa form one 2015 basi pata kwanza shule zako toka mtandaoni kabla hujaenda msimbazi centre kuchukua form -kwa wale wa Dar. Ila mwandae kwa kuwa shule nzuri ni competition ya kufa mtu.
 
Kwa wale wanaoifahamu hii shule nasikia iko Mafinga. Ningependa kupata maelezo yake kuhusu ubora wa taaluma, mahali/sehemu ilipo kwa huko Mafinga na kama ni mchanganyiko na mengine mengi. Natanguliza shukrani mbele.

Kitaaluma iko pouwa sana, ni ya wasichana tu, ipo mafinga kijiji cha luganga barabara ya kuelekea mufindi.
 
Kitaaluma iko pouwa sana, ni ya wasichana tu, ipo mafinga kijiji cha luganga barabara ya kuelekea mufindi.

Yap, nime-google na kuipata ipo karibu na Salesians-Don Bosco Seminary, na hata matokeo yake NECTA ni mazuri sana. Mtoto mwenyewe ninayefikiria kumtafutia ni wa kike. Thanks.
 
ni shule nzuri sana inapatika takriban kilm 2 kutoka mafinga mjini !kwa ufupi kama unataka kumpeleka mwanao pale unatakiwa kutuma maombi kabla ya matokeo ya darasa la saba kutoka na kama anahamia ukubali ataanza form one vinginevyo hawapokei na no shule ya wasichana tu na ni miongoni mwa shule bora zinazopatikana mkoa wa iringa
 
cha ziada ni kwamba ni shule ya kikristo so inapokea wakristo tu otherwise kama ni dini nyingine ukubali mwanao kulelewa kwa misingi ya kikrito bro!
 
Kwa wale wanaoifahamu hii shule nasikia iko Mafinga. Ningependa kupata maelezo yake kuhusu ubora wa taaluma, mahali/sehemu ilipo kwa huko Mafinga na kama ni mchanganyiko na mengine mengi. Natanguliza shukrani mbele.

Shule ni nzuri maana iko karibu na boys wa Mafinga Don Bosco hivo hamna kuugua kuchekelea kabisa

Pia aki interact na hawa wa DON Bosco watamsaidia maana wako kati ya best schools matokeo yao waweza cheki kwa google
 
cha ziada ni kwamba ni shule ya kikristo so inapokea wakristo tu otherwise kama ni dini nyingine ukubali mwanao kulelewa kwa misingi ya kikrito bro!

Hilo halina shida mimi pia ni mkristo, thanks mkuu.
 
Shule ni nzuri maana iko karibu na boys wa Mafinga Don Bosco hivo hamna kuugua kuchekelea kabisa

Pia aki interact na hawa wa DON Bosco watamsaidia maana wako kati ya best schools matokeo yao waweza cheki kwa google

Thanks mkuu, ila hapo kwenye kua karibu na ''boys wa Don Bosco'' na hasa ulipoweka kipengele cha ''hamna kuugua kuchekelea'' na hizo ''interaction'', nimejikuta mapigo ya moyo yakiongezeka speed. Mkuu ulipita hapo Don Bosco nini? Anyway lakini shule academically (kitaaluma) inaonekana iko juu.
 
Kucheza kibaba na kimama mama mhimu.
 
Yaah nimesoma hapo Don Mafinga na hao wa Bethel tulikuwa tuna interact tu ktk mambo ya dini
Yaah Bethel wako poa pia ni yeye tu kupambana
 
Ngoja nifanye utafiti katika hizo rangi
 
Shule ni nzuri maana iko karibu na boys wa Mafinga Don Bosco hivo hamna kuugua kuchekelea kabisa

Pia aki interact na hawa wa DON Bosco watamsaidia
maana wako kati ya best schools matokeo yao waweza cheki kwa google

hapa mkuu kweli lazima moyo ucheze sarakasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…