sematena
Member
- Jan 2, 2011
- 73
- 35
Toka tarehe 27 October 2023, kampuni ya michezo ya kubashiri betpawa inashindwa kutoa (withdraw) pesa kwa wateja wake.
Changamoto hii mpaka sasa bado ipo, kiasi kwamba kuna baadhi ya wadau wana hofu huenda ikawa ndiyo mwisho wa kampuni hiyo kuwepo hapa Tanzania na pesa zao walizoshinda baada ya kuweka mikeka zikaliwa.
Namba ya bure (toll free - 0800 110 051) ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania inaita tu haipokelewi labda hiyo huduma haipo.
Wahusikia wa kudhibiti michezo ya kubahatisha (Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania) wana taarifa ya tatizo hili la betpawa kwa zaidi ya siku mbili sasa? Au ndiyo mpaka hali iwe siyo hali tena ndiyo tunaamka kutoka kwenye usingizi wa pono?!