SoC02 Betting ni njia sahihi ya kujikwamua kiuchumi?

SoC02 Betting ni njia sahihi ya kujikwamua kiuchumi?

Stories of Change - 2022 Competition

KyelaBoy360

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
3
Reaction score
3
Kizazi cha sasa hasa kwa vijana (wasichana kwa wavulana) asilimia kubwa wamekuwa wakijikita katika michezo ya kubahatisha (betting) kama njia ya kujipatia kipato ya haraka,


images (2).jpeg

Picha: Watanzania wakiwa katika moja ya kampuni la michezo ya kubahatisha (Benjamin Fernandez 2017) Lakini swali la kujiuliza Je kweli hii njia ni sahihi na kama inafaida kiasi iko kwa wachezaji mbona makampuni yanazidi kujitokeza kila siku?. Mchezo huu una manufaa zaidi kwa makampuni lakini inazidi kumkandamiza zaidi kijana wa taifa la leo kwasababu
  • Inamfanya awe mvivu wa kufikiri na kupenda njia rahisi ili kupata pesa​
  • Inampotezea mda mwingi wa kushinda mitandaoni kuchambua mechi​
  • Inachochea wizi katika jamii endapo muathirika wa mchezo huu atakosa pesa ya kucheza basi atalazimika kuiba ili tu atimize dhamira ya nafsi yake​
Nini kifanyike kuokoa nguvu kazi ya vijana inayopotea kwaajili ya michezo ya kubahatisha​
  1. Wazazi wafuatilie mienendo ya watoto wao tangu wakiwa wadogo na kuwaweka wazi juu ya madhara ya michezo ya kubahatisha​
  2. Serikali iunde sera mathubuti pia kuwekeza kwa vijana kifedha na vifaa ili waweze kujikita kwenye shughuli nyingine za uzalishaji​
  3. Mwisho, vijana wenyewe tuamke na kuwaza jinsi bora ya kujikwamua kiuchumi.​
 
Upvote 5
Back
Top Bottom