Mmh, Beyonce naye anapenda atensheni na kujulikana kwa Michele.
Upande wa pili, Michele anaonekana anajitahidi sana kubalansi mambo ya umaarufu na familia yake.
Lakini cha tatu, she is just a first lady, ana muda wote wa kumtosha bila kujali kusaidia kuongeza kipato, kwani anafanya kazi gani kwa sasa? Ni mama wa nyumbani tu. Akina mama wengi wa nyumbani huwa wanawajibika sana na familia zao na mambo ya jamii inayozunguka. Sijui kuna msiba kwa jirani anamwakilisha mumewe, sijui kufuatilia watoto shule na kazi zote. Kwa hiyo Michelle naye ni mama wa nyumbani, anahudumia jamii inayomzunguka kupitia u first lady.
Kasheshe ni hawa wanawake wanaofanya kazi, wapo baadhi wanaoweza kubalansi lakini wapo pia wanaoshindwa. Akina baba nao ukute hata hawasapoti familia inabidi mama ndio achakarike, unadhani atapata muda wa kukonsentreti na familia zaidi au jamii inayomzunguka? Kuna akina mama saa 11 alfajiri wako Feri kulangua samaki, jioni wako gengeni kuuza samaki wao, nyumbani wanaonekana saa 3 au nne usiku. Walaumiwe kwa kujaribu angalau kupata mlo wa watoto wao? Kwani wao hawapendi kuwa na waume wanaowaletea kila kitu ndani na wao wakabaki kupaka wanja tu?
Lakini nafasi ya mume kumuwezesha mwanamke kutilia mkazo kwenye familia hasa mme mwenyewe na watoto. Sasa ukute mume leo umemfuna na Kidawa, kesho Havintishi, kwa nini naye asitafute Juma apunguze machungu?