Beyonce writes a letter thanking Michelle Obama for being a role model

Beyonce writes a letter thanking Michelle Obama for being a role model

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
beyonce-obamaconcert-read.jpg

Beyonce-MIchelle-Obama.jpg
 
Mtambuzi, baadhi wanaangalia mwandiko, lakini barua hii imebeba ujumbe mzito kuliko mwandiko wenyewe! Nilivyoisoma hiyo barua, Beyonce anamsifu Michelle kuwa pamoja na ukweli kwamba yeye ni first lady, lakini bado amebaki kama mama mwenye mapenzi ya dhati na anajinyenyekeza ndani ya familia bila kujali wadhifa alionao. Anaihudumia familia yake kana kwamba ni mke mwenye wadhifa wa kawaida. Ni funzo kwa viongozi wengine wenye nyadhifa kama hizo au zinazofanana na hizo!

Si jambo rahisi kwa viongozi wengi wa kike wa cheo chake ambao wamewahi kushuka na kutunza familia zao kwa kiwango alichokionyesha huyu mama. Nafikiri pia kwa muonekano hata mumewe ni mfano mzuri wa kumjali mkewe na ndiyo maana muda mwingi wanapotembea huonyesha mapenzi ya namna fulani. Kwa nje wanaonyesha ni mfano mzuri wa ndoa zenye furaha za kuigwa.

Nawatakia kheri wanandoa hao!

Hapa copy kwa: Kongosho, Nivea, charminglady, Mr Rocky, Eiyer, snowhite, SnowBall, neggirl
 
HorsePower niliangalia mwandiko na zaidi mwandiko uliobeba ujumbe mzito wa maana halisi mtu anayepewa heshima ya kuwa mama bora na mke bora licha ya majukumu na nafasi aliyo nayo
Asante kwa kunikumbusha zaidi niusome tena na tena kupata kile kilichobebwa na ujumbe huo wa Beyonce
 
Last edited by a moderator:
I love that family. Urais pembeni

Alivyokuja hapa alikuwa anakamata mauono ya mkewe wazi wasi, nikajiuliza mbona Ankal wetu hafanyi ivo ivo?

Kaizer wewe ni mchokozi, unauliza nani hafanyi hivyo? Ila ukweli uko pale pale, huwa nahisi ni mfano wa ndoa ya kuigwa!
 
Inawezekana Obama akawa miongoni mwa wanaume wenye furaha sana hapa duniani.

Hata stori ya mapenzi yao jinsi ilivyoanza na waliyopitia inavutia sana.

Beyonce katoa sifa stahiki kwa FIRST LADY, na ni haki kabisa kumfanya role model wake!
 
Mmh, Beyonce naye anapenda atensheni na kujulikana kwa Michele.

Upande wa pili, Michele anaonekana anajitahidi sana kubalansi mambo ya umaarufu na familia yake.

Lakini cha tatu, she is just a first lady, ana muda wote wa kumtosha bila kujali kusaidia kuongeza kipato, kwani anafanya kazi gani kwa sasa? Ni mama wa nyumbani tu. Akina mama wengi wa nyumbani huwa wanawajibika sana na familia zao na mambo ya jamii inayozunguka. Sijui kuna msiba kwa jirani anamwakilisha mumewe, sijui kufuatilia watoto shule na kazi zote. Kwa hiyo Michelle naye ni mama wa nyumbani, anahudumia jamii inayomzunguka kupitia u first lady.

Kasheshe ni hawa wanawake wanaofanya kazi, wapo baadhi wanaoweza kubalansi lakini wapo pia wanaoshindwa. Akina baba nao ukute hata hawasapoti familia inabidi mama ndio achakarike, unadhani atapata muda wa kukonsentreti na familia zaidi au jamii inayomzunguka? Kuna akina mama saa 11 alfajiri wako Feri kulangua samaki, jioni wako gengeni kuuza samaki wao, nyumbani wanaonekana saa 3 au nne usiku. Walaumiwe kwa kujaribu angalau kupata mlo wa watoto wao? Kwani wao hawapendi kuwa na waume wanaowaletea kila kitu ndani na wao wakabaki kupaka wanja tu?

Lakini nafasi ya mume kumuwezesha mwanamke kutilia mkazo kwenye familia hasa mme mwenyewe na watoto. Sasa ukute mume leo umemfuna na Kidawa, kesho Havintishi, kwa nini naye asitafute Juma apunguze machungu?
 
mmmmh.. Kongosho apo napata wasi wasi kama kweli 'ni maam wanyumbani tu' nadhani ana maissue kibao ya kikazi ya kifrst lady anatakiwa atimize......ma functions, meetings, nk...yuko busy mbaya

Ngoja wataalam waje hapa wa mambo ya marekani kina Nyani Ngabu ivi, japo najua ni mrepublican huyu, na wengineo
 
Last edited by a moderator:
I love that family. Urais pembeni

Alivyokuja hapa alikuwa anakamata mauono ya mkewe wazi wasi, nikajiuliza mbona Ankal wetu hafanyi ivo ivo?

unataka nyumba ndogo zake zinune?
 
Ankal...... mi nilitegemewa walau kipindi kile tuone au itakuwa labda hairuhusiwi kidini?

Heeee, weweeeee! unamaanisha amshike mamaa nani yuleeee, kiuno? Mweeee! Si itakuwa ni stori kwenye magazeti yote ya udaku? Uliwahi kuona kiongozi yeyote yule hapa TZ anafanya hayo?
 
Ngoja wataalam waje hapa wa mambo ya marekani kina Nyani Ngabu ivi, japo najua ni mrepublican huyu, na wengineo

Hey, hey, hey....I'm neither a Republican nor a Democrat.

I'm neither strictly conservative nor strictly liberal in my views.

I'm fiscally conservative, socially responsible, and personally accountable type of fella.

So what am I? Perhaps betwixt and between.
 
Lakini HorsePower si ukishamuoa unaruhusiwa kufanya lolote lile linaloruhusiwa mbele za watu kama kumshika kiuno, kumbusu na kumkumbatia na mengine kama hayo wanaogopa nini au tatizo ni zile nyumba ndogo zitaona wivu na kuleta kasheshe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom