Mba Ta Sanja
JF-Expert Member
- Aug 31, 2015
- 383
- 44
Mbona picha ya kuchorwa?usipate tabu...huyo hapo bibi harusi
mtarajiwa aliyezua songombingo ....
![]()
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona picha ya kuchorwa?usipate tabu...huyo hapo bibi harusi
mtarajiwa aliyezua songombingo ....
![]()
Ila my kaka ujue kuna Vitu vingine ni kujitafutia laana tu. Hivi mtu tangu mpo kwenye urafiki unaona kabisa hii issue ni maji marefu kwangu, but unapiga kimya tu. Hadi mtu anaenda kujitambulisha kwenu unamruhusu tu, hadi kutoa posa jamani upo tu, hadi send off then siku ya kufunga ndoa ndo unatoroka. Me mbona ningemtafutia tu sababu ya kumuacha mapemaaa kwenye ushkaji. Amemuumiza sana kisaikolojia kaka wa watu, amewasababishia ndugu Usumbufu bado gharama walizoingia mmh
[emoji87] [emoji87] [emoji85] [emoji85] [emoji86] [emoji86]Haaaaa nimecheka sana nilipofika hapo kwa red kabla hata sijamaliza kusoma ulichoandika!!!!
Huyo bibi harusi ananipa impression ya double dealer.Si ajabu
alikuwa na mwanaume mwingine walioahidiana kuoana na alipoona familia
ya Machange inaharakisha harusi, mdada kachanganyikiwa!
Ndio nn umeandika Heaven Sent?
Mmmmh kwaiyo alivyopanda gari la abilia kuelekea mosh mjini alikuwa bado amevaa shela???
Pole yake, Bwana Harusi ajibu mashitaka maana anajua tatizo.
na nyie wanaume muwage mnasema ukweli ili sisi tuwe huru.
Hayo yanatokea, Mke wangu siku moja kabla ya ndoa alikuwa mkali kwangu kupindikua, alivyotulizwa nami pia kuanza kumfokea akanyamaza, kumbe alikuwa anapanga kutoroka Usiku. Alimshirikisha mpambe wake mmoja ambaye hakukubaliana naye hivyo kiripoti kwa Mchungaji wake, naye alimtaka kuonana naye Usiku ule na kufanya naye maombi. Asubuhi akarudisha Upendo akapekekwa saluni Jioni Ndoa. Amekuja kunihadithia baada ya siku tatu, mpaka Leo hajui kilichokuwa kinampelekesha! Wote tunahisi x-relation either parts zili influence remotely! Maombi jamani, wengime wameolewa na majini hivyo yana wivu!
ok Bado ya bwana wake sasa"
🤣🤣🤣🤣 Daaah inachekesha aseeNi yule Bi harusi aliyetoroka akiwa saloon sasa amepatikana mkoani Arusha, na hali yake haikuwa nzuri alikuwa anaweweseka, habari zinadi kwamba anapatiwa matibabu Selian hospital, Doroth Msuya ( Kulia )
Moshi. Bibi harusi Doroth Msuya aliyetoroka saluni akipambwa saa tatu kabla ya kufungwa kwa harusi yao na kumwacha solemba bwana harusi, Joseph Machange amepatikana jijini Arusha.
Polisi mkoani Kilimanjaro imesema binti huyo hakutekwa nyara kama ambavyo wanafamilia walitoa taarifa Kituo cha Polisi Himo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema jana kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa bibi harusi huyo hakuwa ametekwa nyara. Polisi walifungua jalada la uchunguzi na ilibainika kuwa taarifa za kutekwa zilizokuwa zimetolewa hazikuwa na ukweli, bali aliondoka kwa kupanda pikipiki, alisema.
Kamanda Ngonyani alisema uchunguzi huo ulibaini kuwa wakati akipambwa, aliomba kwenda kujisaidia na baadaye kuomba apelekewe kanga na tishu lakini akatumia mwanya huo kuondoka, alisema.
Alisema uchunguzi huo umebaini kuwa baada ya kupanda pikipiki ilimpeleka hadi kituo cha mabasi na alimlipa dereva wa bodaboda kisha alipanda gari la abiria lililompeleka hadi mjini Moshi.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita saa 6.30 mchana eneo la Lole huko Mwika, Moshi wakati bibi harusi huyo alipotoroka saluni akimwacha mpambe wake akiendelea kupambwa.
Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa tisa alasiri katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Lole Dayosisi ya Kaskazini na baadaye sherehe ingefanyika katika Ukumbi wa Mamba Complex.
Habari zilizopatikana jana kutoka kwa familia ya Machange, zilieleza kuwa Doroth alipatikana juzi baada ya kuonekana akiweweseka, kisha akapelekwa hospitali ya Seliani kwa matibabu.
Ndugu wa karibu wa familia ya Machange ambaye aliomba jina lake lisitajwe, alisema kulikuwa na kikao kilichokuwa kikiendelea kati ya familia ya Machange na Msuya.
Jana (juzi) tulipigiwa simu na kuelezwa kuwa Doroth amepatikana Arusha lakini yuko kama hajielewielewi na hajui nini kimetokea, Alisema.
Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo, zinadai kuwa bibi harusi huyo alikuwa ametaka harusi hiyo iahirishwe na ombi hilo alilitoa zaidi ya mara 10 bila kueleza sababu.
Nooibra87 hope umesoma comments za humu na umejifunza kitu shem