Singo Batan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 295
- 198
Nchi ya Kenya inatarajia kufanya uchaguzi wa Rais wa awamu ya 5 mapema mwezi Agosti 2022. Duru za uchaguzi zinaonesha kumpa nafasi zaidi Bwana Raila Odinga ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Idadi kubwa ya Wapiga kura wa Kenya, wana imani zaidi na kambi ya Mzee Raila sio kwasababu ya ubora wa sera zake, bali watu wanaomzunguka ambao ni wanasiasa wenye nguvu na ushawishi mkubwa.
Mmoja wa wana siasa hao ni Bi. Martha Karua, Mgombea mwenza katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Kenya.
Kwa Maoni ya wakenya wengi wanaamini Bi. Martha anaweza kuwa Rais wa Nchi hata kama Raila hayupo. Na wanakiri kwamba kifo cha Dr. John Magufuli kwao kilikuwa ni fundisho muhimu katika kufanya maamuzi ya nani awe Rais.
Bi Martha anaondoka na kijiji cha wapiga kura na kumfanya Raila afanye kampeni za kurelax sana.
Pamoja na Bi. Martha yupo fundi mwingine wa kupanga maneno anaitwa Bw. Peter Kenneth, kampeni meneja wa team Raila. Ambaye anapiga backup kubwa sana kwa wagombea wake.
Upande wa Bw. Ruto anapambana sana na Raila, na amemsahau injinia atakayejaza masanduku ya kura ambaye ni Bi. Martha.