Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kuna mtu kaniletea makala ya Bi. Titi Mohamed na akaniuliza usahihi
wa makala hiyo.
Nimeisoma na mimi nikawa mwanafunzi makala ina mengi ambayo
kwangu sikuyajua kwa undani wa kiasi kilichoandikwa mle.
Kwa kuonyesha shukurani zangu kwa huyu ndugu yangu nami nikaona
nimuonyeshe niliyopata kuandika kuhusu Bi. Titi Mohamed na wazalendo
wenzake waliopigania uhuru pamoja na yeye.
Hapo chini ni mazungumzo yetu:
Naomba kujuwa kama hizi taarifa zinazo sambaa kwenye Mitandao za Bibi Titi ziko Sahihi.
BIBI TITI MOHAMED: MWANAMAMA SHUPAVU NA MPIGANIA UHURU HODARI ALIYETINGISHA NA KUHESHIMIKA AFRIKA MASHARIKI NZIMA!!!
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said:
1. Usuli:
1.1 TITI Kuzaliwa:
TITI MOHAMED SALUM MANDWAGA alizaliwa mwezi Juni 1926 jijini Dsm.
1.2 Wazazi Wa TITI: Baba yake aliitwa Bw. MOHAMED BIN SALIM na mama yake aliitwa Bi. HADIJA BINTI SALIM. Wazazi hawa walitokea Rufiji.
Baba yake alikuwa mfanyabiashara ya mbuzi na ng'ombe na mama yake alikuwa mkulima.
2. Elimu:
2.1 Baba Agoma TITI Asisome:
Baba yake alikataa katukatu kwamba TITI asisome shule kwa hofu angekuwa kafiri.
2.2 Mama Ampeleka TITI Shule:
Baba yake alifariki TITI akiwa na miaka 9 tu. Mamaye akatumia fursa hiyo kumpeleka TITI Shule ya Wasichana Uhuru ambako alisoma hadi darasa la 4.
3. TITI Aolewa na MHENGA akiwa na miaka 14 tu:
TITI aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu.
4. TITI Ajifungua Mtoto wa Kike:
TITI alijifungua mtoto wa kike aitwae HALIambaye alikuja kuolewa na MZEE IDD HAMIS, Mshambuliaji hatari wa Cosmopolitans, klabu ya kwanza kutwaa ubingwa TZ ambapo walikuwa wakiishi mtaa wa Skukuu na Udowe na kubahatika kupata watoto 3 wa kiume.
4. TITI Aachana na mumewe:
TITI aliachana na mume huyo kijeba ambaye alikuwa ni baba wa HALIMA , mume ambaye hakuwa chaguo lake.
5. TITI Awa Maarufu kwa ngoma za Maulid:
TITI alianza kuwa maarufu angali mdogo alipokuwa kiongozi wa ngoma za maulid ambazo zilimjenga uwezo wa kujiamini na hivyo akawa maarufu sana.
6. TITI Aolewa na BOI SELEMAN:
TITI aliolewa na dreva wa teksi aitwae Boi Selemani, baada ya ndoa yake ya kwanza kusambaratika.
6. TITI Ajiunga na TANU:
TANU ilizaliwa tarehe 7.7.1954. Wanachama wa mwanzo kupata kadi za TANU walikuwa NYERERE(Kadi na.1), A. SYKES Na.2, A. SYSKES No.3 D. AZZIZ No.4, DENIS PHOMBEAH No.5, DOME OKOCH Na.6, J. RUPIA Na.7.
Bw. BOI, mme wa TITI, alikuwa ni rafiki wa Bw. SCHNEIDER PLANTAN aliyekuwa mmoja wa viongozi wa TAA. Siku moja, Bw. PLANTAN alienda nyumbani kwa BOI na kumweleza kuwa ametumwa kumweleza TITI ajiunge na TANU.
BOI alikubali na akajinunulia kadi na.15 ya TANU na pia akamnunulia TITI kadi na.16. Jumla alitoa TZS 12/= kwani kila kadi iliuzwa TZS 6/=.Ndivyo walivyojiunga TANU. BOI pia alichangia TSH 10/= kwa ajili ya nauli ya Mwalimu NYERERE kwenda UNO (TSH 5/= kila mmoja).
7. TITI Asomba wamama Lukuki Kujiunga TANU!!!
Tarehe 8.7.1955, TITI akiwa Mwenyekiti wa Tawi la Wanawake wa TANU, alifanya mkutano mkubwa na kuvuna wanachama 400 na ndani ya miezi 3 tu akawa amepata wanachama 5,000:
"Nilizungumza na mama Swalehe Kubunju, Kiongozi wa "Tongakusema" na akawaita wakinamama wote wa Tongakusema. Nikakutana nao Livingstone street alikokuwa akiishi mama Kubunju ambaye alihimiza: -"Ewe mwanamke, TITI anakuita, TITI yuko hapa". Hivyo wamama wakawa wanakuja kirahisi. Wakija nikawa nawaambia tunataka uhuru lakini hatuwezi kuupata kabla ya kujiunga TANU. Wanawake ndio nguvu ya dunia, hawa wan…
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Hujanisumbua dada yangu nimefurahi sana kumsoma Bi. Titi. Historia uliyoleta haina shaka nami In Shaa Alkah nitakuletea niliyoandika kuhusu Bi. Titi.
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Mohamed Said: TAMTHILIA YA BIBI TITI MOHAMED NA PROF. EMMANUEL MBOGO
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Mohamed Said: Bibi Titi Mohamed (1926 - 2000) Shujaa wa Uhuru wa Tanganyika
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Ukipenda kumsoma Bi. Titi historia yake yote katika uhuru wa Tanganyika soma kitabu hiki:
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Shukran kwa maelezo
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Miaka ya 1990kati, nikiwa Mwanachama wa Tamwa na Wenzangu nilibahatika kuwa karibu naye na kupata baadhi ya Mambo yake wakati wa Uhuru na Mwl Nyerere (Yeye alikuwa akimwita Julius)
Nilikuwa na tape zenye sauti yake lakini zimepotea au kuharibika😭
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Andika kuhusu mazungumzo yenu ni kitabu kizuri kitakuwa. Niamini!
Independence Ball Diamond Jubilee Hall muziki ulipigwa na Royal Marine Band
Bi. Titi na Nyerere Viwanja Vya Jangwani 1950s
Pembeni ya Bi. Titi ni mwanae Halima.
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: TANU Branch Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu hili tawi alilianzisha Ali Msham 1955.
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Pamoja na kumbukumbu ya Hao Watu nimeiona Dar yetu ilivyokuwa Mabati ya siku hizo😜
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Umejaaliwa Hazina kubwa Sanaaaaa ya Historian ya Nchi hii
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Naomba kama utaweza Mtafute N. KAISI ana mengi ya Nchi hii
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Mohamed Said: PICHA ADIMU ZA TANU, JULIUS NYERERE NA WAZALENDO WALIOSAHAULIKA KATIKA HISTORIA YA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Mimi ndiye mtafiti peke yangu ukimtoa John Iliffe wa Cambridge aliyebahatika kusoma Nyaraka za Sykes Family zenye historia inayoanza mwishoni 1800 hadi kufikia uhuri 1961.
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Simjui Bwana Kaisi tafadhali muonyeshe kitabu changu kwanza.
[11:42 PM, 2/21/2019] Mohamed Said: Kwa Sasa sijuwi anapatikana wapi, ila nilibahatika kukutana nae Nyumbani kwa Mzee Wetu Kitwana Kondo(Mwenyezi Mungu Amrahamu) nikasikia Simulizi zao za Ujana/Siasa /Harakati za Uhuru wa Tanganyika.
In Shaa Allah itaendelea...