Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mwanamke jasiri na mwenye maono mapana ya maendeleo, Bi. Valeriana Pascale Itovagonze, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu 2025.
Akizungumza na Nurudigital leo 27 Juni 2025 , Bi. Valeriana amesem kuwa amechukua hatua hiyo baada ya chama chake kuruhusu rasmi wanachama kuanza kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo ubunge.
“Nimeamua kugombea kwa sababu naamini ninao uwezo, nia na uthubutu wa kulitumikia Jimbo la Karenga kwa uadilifu na moyo wa uzalendo. Nina maono ya kuona Karenga inapata maendeleo ya kweli kwa kushirikisha wananchi wote,” amesema Bi. Valeriana.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akiwa ni mmoja wa wanawake waliopata msukumo kutoka kwa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Bi. Valeriana ameeleza jinsi Rais Samia alivyoamsha ari ya wanawake nchini.
“Mheshimiwa Rais wetu ameonyesha mfano wa uongozi wa hali ya juu. Amefungua milango kwa wanawake, ametupa ujasiri, na sasa hatuogopi tena kushiriki kwenye nafasi za maamuzi. Ni wakati wetu kuendelea kazi hii nzuri,” amongeza.