Mkuu hilo si kosa lake ni kosa la kimfumo kwa Watanzania wengi. Watanzania tulio wengi hatukuzoeshwa kwenye maisha ya kujiajiri, tunapenda kuajiriwa. Ni muhimu sasa tukaanza kubadili mind set zetu kwa kuwaza zaidi kujiajiri. Ukitaka somo la kujiajiri nenda Wilaya ya Makete (ingawa wengi tumeaminishwa ni uchawi), utaona vijana wengi kule wanaanza na mitaji midogo ya sh 100,000 either kwa kulima viazi au kununua miti na baadaye kuwa wasafirishaji wakubwa wa mbao. Akiona mtaji unakuwa mkubwa anafanya biashara upande mwingine analima. Ndio matajiri wa Makete wanavyopata utajiri. Ila kujinyima (kutofanya anasa) ni sehemu mojawapo ya falsafa yao ya kufanikiwa kibiashara.