Biashara ambazo hali ishakuwa mbaya kipindi hichi cha Corona

Sawa mkuu.
 
Kampuni za ukaguzi wa mahesabu - wakaguliwa wameji "LOCKDOWN" majumbani mwao
 
Oh nilifikiri una mbinu mbadala kumbe mbinu unayoisema ni kuvunja sheria. Faini yake ni 30,000/-. Kilwa road nilishakuta traffic anasimamisha daladala moja moja wanakagua. Unafikiri huu uvunjaji wa sheria dereva ataufanya kila siku kila trip?
hata kabla ya level seat biashara ya daladala inaendeshwa na uvunjaji wa sheria
 
Aisee mwenzenu Mimi toka juzi nimefungiwa pooltable Sasa ndo ilikuwa inaniweka mjini kwa Siku nilikuwa siwezi kukosa elfu kumi na tano 15,000 kwenda juu Sasa nimefungiwa Na cjui ni lini covid19 itaisha cha kushangaza ni kwamba pooltable wanafungia muda huo bar, grocery wanaziacha wakat kule ndo hatar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu! Ilibidi hata bar na kumbi za starehe zifungwe kabisa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…