Ngoja nikushauri kitu mdogo wangu coz sisi tumepia vyuoni kama wewe,unaweza ukadharau hii biashara but amini nakuambia unaweza ukawa kila siku unatoka na 20,000/
Tafuta Kibegi cha mgongoni nenda kwenye maduka ya jumla nunua pipi zile za kisista duu yani pipi kijiti au hata ivory,gum like Batook,n.k,vocha za kukwangua na kurusha,biskuti,karanga,tambi na hata ubuyu.then uwe unazunguka campus amini utauza sana coz maeneo mengi ya chuo biashara hizi hazipo ndani ya maeneo ya chuo(hawaruhusu machinga kuingia chuoni).sasa kwa vile watu ni wavivu kuvuka kutembea kufata pipi au biskuti au vocha we utatumia advantage hiyo kupiga salio.
Biashara za kipuuzi ndo zinalipa sana bora tu usiwe na aibu,uzuri wa biashara hii ni kwamba haiitaji usimamizi ofisi ni mgongoni mwako,haili muda wako wa masomo,unaweza kuifanya hata darasani wakati lecture inaendelea,haina usumbufu wa TRA,easy to carry,watu wakishakuzoea ndo nafasi yako nzuri ya kupiga hatua 1000 ahead!
kila la heri!!