Biashara au ujuzi kipi bora kwa msichana wangu wa kazi?

Penelope

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
713
Reaction score
642
Habari Jf,

Nina msichana wangu wa nyumbani ambaye kwa kweli amenisaidia sana kwa miaka 2 na nusu aliyokaa na mimi.pamoja na kazi zake kufanya vizuri lakini pia hana kiburi au tabia za kuchocha mtu.sasa anataka kwenda kwao dec mwaka huu na asilimia 98% ya mshahara wake nimemuhifadhia nitampa siku anaondoka,,ingawa anasema atarudi hapo sina uhakika.kwao ni Singida.

Sasa nawaza kama akirudi,natamani nimsaidie na nimshauri asomee kitu kitakacho kuja kumpa ajira nyingine badae,, kwa level yake ya elimu ni darasa la 7..naomba mnishauri ujuzi gani anaweza kusomea ila cherahani mwenyewe hapendi..

Au hela atakayopata na kama hatarudi kwangu biashara gani anaweza kufanya ingawa hapa kwenye biashara napata mashaka kama atamudu..ana miaka 20
 
muulize anahitaji fani gani? kisha mpeleke akapate ujuzi..
 
Mimi nimempata mmoja week chache sana, anatokea Dar.. Ndio kazaliwa hapa hapa Dar, alifaulu standard seven na anataka kushona. Nimemshauri asome QT ili afanye Necta kwanza.
 
Mimi nimempata mmoja week chache sana, anatokea Dar.. Ndio kazaliwa hapa hapa Dar, alifaulu standard seven na anataka kushona. Nimemshauri asome QT ili afanye Necta kwanza.
na mimi niliwaza suala la qt,sababu siku zijazo chet cha form 4 ni muhimu sana
 
Mimi nimempata mmoja week chache sana, anatokea Dar.. Ndio kazaliwa hapa hapa Dar, alifaulu standard seven na anataka kushona. Nimemshauri asome QT ili afanye Necta kwanza.
Afany3 necta ili iweje? apate cheti? ili iweje?

mtu anataka kujiajiri mnakomaa na QT hivi still mnaamini vyeti ndo mafanikio?

Acha afanye anacho penda na achaba na Mindset za vyeti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Elimu ya Std 7 sidhani kama ni vizuri akisomea ufundi, nadhani umsaidie aanze QT, amalize form 4 au akiweza form 6 ni vizuri zaidi, kisha mpeleke kozi ya AVIATION, ni kozi nzuri na ajira zipo.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimempata mmoja week chache sana, anatokea Dar.. Ndio kazaliwa hapa hapa Dar, kalifaulu standard seven na anataka kushona. Nimemshauri asome QT ili afanye Necta kwanza.

Mnawapoteza hao watoto nyie, mambo ya QT sio lazima , na anaweza feli akawa amepoteza time yake., Cha msingi wapigisheni short courses za mambo madogo wanayoweza kujiajiri na ujasiriamali wakapambane. Mf kuna short courses za utengenezaji wa cosmetics, sabuni, kilimo biashara, etc etc.

na mimi niliwaza suala la qt,sababu siku zijazo chet cha form 4 ni muhimu sana
 

ni wazo zuri pia lakini huoni akipata chet cha form iv halafu akichanganya na ujuzi wa jambo fulani atakua vizuri zaidi,,sababu bado umri unaruhusu..
 
ni wazo zuri pia lakini huoni akipata chet cha form iv halafu akichanganya na ujuzi wa jambo fulani atakua vizuri zaidi,,sababu bado umri unaruhusu..


Atakuwa chini ya uangalizi wako muda huo wote.? Anyway labda aende huko shule kwa lengo la kupata exposure maybe ila kwa lengo la kusoma na kufaulu mtachemka, mtu ukishakaa kitaa kwa muda then urudi shule, akili nyingi huwa dormant.

Ningekushauri kama unataka akasome tena, mpeleke english course ya ukweli sio ya kibabaishaji, akaijue lugha vizuri , mengine hayana maana mi naona. hiyo ndo exposure ya muhimu anayoihitaji, baadae akifakiwa akiona shule ina umuhimu atarudi mwenyewe.
 
[emoji121]
MKUU,
HIYO HELA ULIYOMTUNZIA KIASI GANI?

JIBU LITASAIDIA KUTOA USHAURI WENYE TIJA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nilikaa mtaani muda mrefu sana kama miaka kumi hivi nikaamua kwa hela yangu ndogo kusoma english course baadaye nikaanza QT kwa kusoma mimi na mwalimu tu wa somo husika nikafanya mitihani nikafeli ya form two nikarudia nikafaulu, nikafanya ya form four nikapata pass zangu nikarudia tena, sasa najielewa hata huyo mtoto ataweza tu akitaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…