SoC01 Biashara: Changamoto wanazokabiliana nazo Watanzania

SoC01 Biashara: Changamoto wanazokabiliana nazo Watanzania

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 13, 2021
Posts
7
Reaction score
5
Sekta ya biashara nchini inakabiliwa na changamoto kadhaa wa kadhaa ambazo inazorotesha utendaji na ufanisi katika sekta hizo. Miongoni mwa changamoto hizo ambazo bahati nzuri serikali ya awamu ya sita imeweza kuzibaini na kuzipatia ufumbuzi ni suala la mgogoro wa kibiashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo bidhaa za wakulima kutoka Tanzania zimekuwa zikizuiliwa kuingia Kenya.

Hii inazorotesha ufanisi na ukuaji wa nchi yetu. Tunahitaji Tanzania kuwa ni nchi ambayo si itaweza kuuza mazao ya biashara nje ila Tanzania itakayoweza kuuza bidhaa za chakula kwa majirani zake. Tunahitaji kuboresha mazao yetu kwa kuongeza uzalishaji na kuyasindika ili tuyape thamani zaidi.

Mbali na yote hayo ni lazima tuwe na miradi ya kimikakati ambayo itaweza kuzalisha ajira na kuimarisha biashara nchini.

Tanzania tumebarikiwa kubwa na bahari lakini bado hatujaitumia vyema ni lazima tuwe na bandari kubwa na bora ili Tanzania iwe ni kitovu cha biashara katika ukanda huu wa afrika mashariki.

Mfano mzuri ni Ethiopia baada ya kujijua kuwa hawana bahari wakaamua kuanzisha uchumi wa ndege kwa kuanzisha shirika kubwa la ndege katika bara hili la afrika hivyo basi ni lazima Tanzania nayo iweze kua bunifu kwa kutumia vyema kile ilichonacho ikiwemo samaki na mifugo ambapo inaweza kujitangaza na kua mzalishaji mkubwa wa nyama na samaki afrika na duniani,tuna mifugo na samaki wa kutosha halafu hatujui vyanzo vipya vya mapato ni vipi.

Ni vyema kukaribisha sekta ya binafsi ili kukuza na kuinua uchumi wetu ila kwa pale penye uwezo ni vyema zaid tukawapa kipaumbele wawekezaji wetu wa ndani ili kuwainua na kuimarisha uchumi miongoni mwetu, tunaposema biashara na uchumi tunamaanisha roho ya nchi yetu ni lazima tuwe na kodi zenye kueleweka mfano kodi ya mgeni anaishi kwa salama na amani nchini ni lazima alipe kodi katika nchi ili ukarimu na usalama wake vitunzwe zaidi.

Tunahitaji kuwa na kodi ya mashamba makubwa ya mazao ya biashara kutoka kwa wamiliki,tunahitaji kodi ya mwaka kwa kila mfanyabiashara mkubwa pesa zake zikifikia kiwango fulani ili utajiri wake ule anaozalishiwa na wafanyakazi wake kila siku ya mungu mwisho wa mwaka sehem ndogo ya jasho lile liende nikamnufaishe masikini moja kwa moja ili aende akafanye miradi na kumkomboa na umasikini.

Tunahitaji kuondoa riba ama kupunguza kwa asilimia kubwa ili mwananchi akakomboke mfumo uliopo hivi sasa ni maskini anapo kopa huzidi kufukarika na kuinufaisha bank hata ile faida ndogo anayoipata huwa haitoshi kutokana na ziada ya fedha anayorejesha na akishindwa kulipa kwa wakati huuzwa hata kile kidogo alichonacho na kubakia fukara zaid,ili tuwe na uchumi bora ni lazima turekebishe mfumo wetu wa mabenki.

Mwisho kwa kumalizia naweza sema changamoto za biashara pamoja na uchumi zipo nyingi ila tunaweza kurekebisha hilo kwa kuhakikisha tuna wathamini wananchi wetu,ukitoa masoko ya kimataifa ni lazima tulikuze kwanza soko letu la ndani kwa kuwawezesha wajasiriamali wetu na kuwaondolea ugumu wa maisha wananchi wetu kwa kuwapatia huduma nzuri za kijamii pamoja na elimu bora ili waweze kujiajiri na kuajirika na kuinyanyua sarafu yetu. Tupo na madini mengi ipo siku tunaweza kutengeneza hata shilingi ya dhahabu na kuifanya Tanzania iwe na pesa yenye thamani zaid duniani
 
Upvote 5
Back
Top Bottom