Wadau ,
Nimepata fremu maeneo ya kariakoo katika eneo ambalo ni la vitu vya electronics. Sasa niko katika utafiti kujua kipi kinafaa Zaidi kwa biashara kati ya vitu vifuatavyo;
a. Biashara ya kuuza TV, radio na friji kwa wakati mmoja au
b. Biashara ya kuuza simu na vifaa vyake(phone accessories)
c. Biashara ya kuuza spare za simu .
Naomba kwa wale wadau wenye uzoefu na biashara hii , pia kama wanaweza wakanishauri , chochote kile ambacho kinaweza kikaongeza mafanikio katika hili pia nitashukuru.
Asante sana