Biashara gani inamfaa mwanachuo?

Biashara gani inamfaa mwanachuo?

JFMemba

Senior Member
Joined
Jun 28, 2021
Posts
134
Reaction score
247
Habari wakuu

Dogo amechaguliwa kujiunga UDSM (Main Campus). Anataka atakapokuwa chuo awe pia anafanya biashara ndogo ndogo ambayo haitampotezea sana muda wa masomo. Ikiwezekana aifanye mwenyewe au ampe mtu
katika maeneo ya jirani asimamie.

Tayari amejichanga tangu amalize chuo na ana 1.5m na sisi nduguze tumempa 1.2m hivyo ana mtaji wa 2.7m nje ya pesa ya matumizi mengine.

Sasa tunaomba ushauri wenu kwa hiyo 2.7m anaweza kufanya biashara gani angalau ya kumuongezea kipato. Dogo ana asili ya kujituma sana kwenye ujasiriamali.

Ushauri wenu wakuu
 
Achague kimoja
Waliofanikiwa wapo walioacha kusoma na wapo waliosoma. Huo mtaji ni mdogo. Apige desa
 
inategemea una msingi au mtazamo upi kwenye ufanyaji wa biashara ila biashara nzuri kwa mwanachuo ni ile itakayompa muda wa kusoma na hapo hapo wanafunzi wenzake ndo wawe soko lake
 
Anunue printer, binding machine na makorokoro madogo ya stationary awe anaprintia wanafunzi. Anajiunga groups za classes tofauti atangaze hiyo huduma na awe tiyari kupiga kazi usiku. Atakuwa anaprint assignments za wanachuo na akiwa mzoefu baadae ataanza kuprint research ambazo zinahitaji muda kuzipanga.

Kama anachangamka kichwani atajifunza kufanyia watu research, atajua wapi pa kupata machapisho na wapi pa kulipia premium kupata huduma kadhaa ambazo individual hawezi toa hela yake nyingi. Kuna vilaza kibao wanakuja chuo hawataki kuwajibika na wanafaulu kiujanja ujanja. Kazi ya kuprint itategemea anasoma nini maana inakula muda. Atalazimika kukaa karibu na chuo ambako unalipa kodi kubwa.

Hapo kuna hela inabaki aitunze akipata nyingine aongeze aanzishe nail bar. Ataweka kijana wa kufanya kazi aendelee na mambo mengine.
Juice bar naona sio option nzuri kwa sasa.

Au kama vipi kwa sasa angeongeza hela kwenye hiyo 2.7M angenunua simu used za Oppo, Samsung, Google Pixel na iPhone. Hii haitumii sana muda ila asiwe dalali.
Nimetoka chuo last month tu hapo, naongea kwa uzoefu. Kwanza vigumu kushauri mtu from nowhere hujui interest zake wala uwezo wake
 
Asante mkuu
Kitu kingine cha kuzingatia umesema dogo anajituma kwenye ujasiriamali

Ingependeza sana kama akifanya biashara kwa malengo ya muda mrefu yaani biashara ambayo ni multipurpose

target customers wake wawe wanachuo wenzake na ambao sio wanachuo hata akimaliza chuo anaweza Kuendelea nayo

Sio ile amemaliza chuo na biashara ndo inakufa hapo

Ni maoni yangu tu
 
Asante sana mkuu. Hiyo ya simu naona kama anaweza kufanya. Hizo simu anazipata wapi? Msaada plz
 
Kitu kingine cha kuzingatia umesema dogo anajituma kwenye ujasiriamali

Ingependeza sana kama akifanya biashara kwa malengo ya muda mrefu yaani biashara ambayo ni multipurpose

target customers wake wawe wanachuo wenzake na ambao sio wanachuo hata akimaliza chuo anaweza Kuendelea nayo

Sio ile amemaliza chuo na biashara ndo inakufa hapo

Ni maoni yangu tu
Ungetoa mfano wa hiyo biashara mkuu
 
Back
Top Bottom