Anunue printer, binding machine na makorokoro madogo ya stationary awe anaprintia wanafunzi. Anajiunga groups za classes tofauti atangaze hiyo huduma na awe tiyari kupiga kazi usiku. Atakuwa anaprint assignments za wanachuo na akiwa mzoefu baadae ataanza kuprint research ambazo zinahitaji muda kuzipanga.
Kama anachangamka kichwani atajifunza kufanyia watu research, atajua wapi pa kupata machapisho na wapi pa kulipia premium kupata huduma kadhaa ambazo individual hawezi toa hela yake nyingi. Kuna vilaza kibao wanakuja chuo hawataki kuwajibika na wanafaulu kiujanja ujanja. Kazi ya kuprint itategemea anasoma nini maana inakula muda. Atalazimika kukaa karibu na chuo ambako unalipa kodi kubwa.
Hapo kuna hela inabaki aitunze akipata nyingine aongeze aanzishe nail bar. Ataweka kijana wa kufanya kazi aendelee na mambo mengine.
Juice bar naona sio option nzuri kwa sasa.
Au kama vipi kwa sasa angeongeza hela kwenye hiyo 2.7M angenunua simu used za Oppo, Samsung, Google Pixel na iPhone. Hii haitumii sana muda ila asiwe dalali.
Nimetoka chuo last month tu hapo, naongea kwa uzoefu. Kwanza vigumu kushauri mtu from nowhere hujui interest zake wala uwezo wake